Header AD

header ads

KATIBU MKUU UWEKEZAJI,VIWANDA NA BIASHARA ATEMBELEA TANTRADE



Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara *Dkt.Hashil Abdalah* amekutana na timu ya Manejimenti ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) ikiwa ni utaratibu wake wa kukutana na taasisi zilizopo chini ya Wizara.

Dkt.Hashil ameitaka menejimenti kuhakikisha Sekta ya Biashara nchini inakuwa kwa kasi na kuleta matokeo chanya  kwa Taasisi ,Wizara na taifa kwa ujumla.


Dkt.Hashil amesema kuwa ,Tantrade imekuwa taasisi yake ya kwanza kukutana nayo kutokana na majukumu na umuhimu wake kwa Taifa katika kuendeleza Biashara za ndani na nje ya nchi.

Aidha amesisitiza  uwajibikaji na uadilifu  kwa watumishi wote ili kuhakikisha Jamii inapata Huduma Bora na kwa wakati.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Bi.Latifa Khamis amemshukuru Katibu Mkuu kwa 
Kuitembelea  taasisi na ameahidi kuendelea kusimamia majukumu ya taasisi Kwa ufanisi.


KATIBU MKUU UWEKEZAJI,VIWANDA NA BIASHARA ATEMBELEA TANTRADE KATIBU MKUU  UWEKEZAJI,VIWANDA NA BIASHARA  ATEMBELEA TANTRADE Reviewed by Fahadi Msuya on January 16, 2023 Rating: 5