Header AD

header ads

MAOMBI MAALUM YA KUZUIA MADHARA YA MVUA NA MAAFA ZAIDI KWA TAIFA LA MAREKANI



Na Taji Silas

Kanisa la Good News for all Ministry limefanya maombi maalum  ili kuzuia mvua na barafu na  zilizopita kipimo na kuleta maafa katika maeneo mengi ndani ya  nchi ya Marekani yaliyo tokea katika Msimu wa Krismasi na mwaka mpya 

Maombi hayo yameongozwa na Askofu  wa kanisa Hilo Dakta CHARLES GADI Leo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema ni mwendolezo wa maombi yaliyofanyika awali 21/12/2022  yaliolenga kuliombea Taifa Hilo kupata mvua za kutosha.
"Leo tumejitokeza tena hapa kumwomba Mungu illi kuzuia hali hiyo ya maafa na badala yake waendelee kupata mvua za kutosha,na kuondoa madhara yatokanayo na mvua nyingi.Hivyo Leo katika maombi haya turatangaza kukomesha madhara zaidi yanayosababishwa na mvua hizo pamoja na barafu kali, ambayo imeendelea kuwaathiri wananchi wa Taifa Hilo la Marekani katika Msimu huu wa sikukuu za Krismasi na mwaka mpya."

Amesema lengo la kutoa msaada wa maombi kwa Taifa la Marekani ni kurudisha  fadhila kwa Taifa Hilo ambalo liliwai toa msaada wa chakula kwa Tanzania katika kipindi ambacho Nchi ilikua inapitia wakati mgumu wa njaa.

"Hii inaonyesha kuwa katika Dunia hii tunategemeana. Wewe ukiwa na hiki,wenzako wanakuwa na kile na hivyo mwisho tutakuwa tunafaidiana na kusaidiana. Tutaendelea kuombea Taifa Hilo katika sekta mbali mbali ili Mungu aendelee kuwasaidia pale walipopunguka".

 Kufuatia maombi hayo Askofu GADI amezitahadharisha  kampuni mbalimbali  zikiwemo kampuni za vyakula,mavazi  pamoja na Taasisi za serikali za Marekani kujiandaa na  majira maalum ya joto ambapo kanisa Hilo linaamini ni yatakuwa matokeo ya maombi hayo yaliyofanyika leo
MAOMBI MAALUM YA KUZUIA MADHARA YA MVUA NA MAAFA ZAIDI KWA TAIFA LA MAREKANI MAOMBI MAALUM YA KUZUIA MADHARA YA MVUA NA MAAFA ZAIDI KWA TAIFA LA MAREKANI Reviewed by Fahadi Msuya on January 04, 2023 Rating: 5