Header AD

header ads

MILIONI 438,111,518.39 KUNUFAISHA VIKUNDI 24 MIKOPO ASILIMIA 10 MANISPAA YA KIGAMBONI




Hayo yamebainika leo 17/1/2023 wakati wa mahojiano na Mratibu  Dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi  anashughulikia masuala ya mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali katika Idara ya Maendeleo ya jamii Manispaa ya Kigamboni ndg.Masesa Mgonela Luanda ambapo amesema tayari vikundi 24 vilivyokidhi vigezo  vimeshapitishiwa mikopo yao na taratibu zote zimefuatwa hivyo watapokea fedha zao ili kutekeleza yale waliyoyapanga kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za ujasiriamali na kujiinua kiuchumi.

Akichanganua jinsi mgawanyo wa fedha hizo ulivyo kulingana na makundi ndg. Masesa amesema katika fedha hizo shilingi 211,265,411.34 zitaenda kwa vikundi 11 vya wanawake,shilingi milioni 131,265,411.34 zitaenda kwa vikundi 7 vya vijana na shilingi milioni 95,580,695.71 zitaenda kwa vikundi 6 vya watu wenye ulemavu.

Kuhusu urejeshaji wa mikopo hiyo ndugu Masesa anatoa wito kwa wanufaika wa mikopo hii kuwa fedha hizo sio zawadi inatakiwa kurejeshwa ili vikundi vingi zaidi viweze kunufaika kwani pesa zinavyorudi ndivyo zinavyosaidia kuwakopesha wengine na vikundi vingi vinapata kufaidika zaidi.

Mikopo hii ya asilimia kumi isiyo na riba  hutolewa na kila halmashauri ambapo imewanufaisha na kuendelea kuwanufaisha makundi mbalimbali katika kujikwambua kiuchumi ikiwa ni dhamira thabiti ya serikali kuwakwamua wananchi kiuchumi na kuboresha maisha yao pamoja na kutekeleza Ilani ya CCM kivitendo.KAZI IENDELEE

Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini KGMC
MILIONI 438,111,518.39 KUNUFAISHA VIKUNDI 24 MIKOPO ASILIMIA 10 MANISPAA YA KIGAMBONI MILIONI 438,111,518.39 KUNUFAISHA VIKUNDI 24 MIKOPO ASILIMIA 10 MANISPAA YA KIGAMBONI Reviewed by Fahadi Msuya on January 17, 2023 Rating: 5