Header AD

header ads

MUSWADA WA SHERIA YA HABARI KUSOMWA KWA MARA YA KWANZA JANUARI HII



Mwenyekiti wa Jukwaaa la Wahariri Tanzania (TEF), amesema macho na masikio ya wadau wa habari nchini, yanaelekezwa jijini Dodoma kusubiri muswada wa Sheri ya Habari ukisomwa kwa mara ya kwanza Januari hii.

Akizungumza leo tarehe 19 Januari 2023, katika ofisini za TEF, Kisutu jijini Dar es Salaam amesema, muelekeo ni mzuri na maelekezo ya Rais Dkt.  Samia Suluhu yanatekelezwa na shauku wa wadau wa habari kuona mswada huo unaingia bungeni.

Amesema wanatarajia mambo yatakwenda vizuri endapo muswada huo utaingia bungeni na kusomwa kwa mara ya kwanza .

" Wiki hii tunarajia kwamba Wizara ya habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari itawasilisha muswada wa  huduma za habari bungeni na utajadiliwa na mungu akipenda mwezi Febuari utakua umepitishwa kuwa sheria na tumeona kwamba mweleke ni mzuri " amesema Balile 
MUSWADA WA SHERIA YA HABARI KUSOMWA KWA MARA YA KWANZA JANUARI HII MUSWADA WA SHERIA YA HABARI KUSOMWA KWA MARA YA KWANZA JANUARI HII Reviewed by Fahadi Msuya on January 19, 2023 Rating: 5