Header AD

header ads

WAZIRI BALOZI DKT. CHANA AHIMIZA UWEKEZAJI NA UBORA KWENYE SEKTA YA UTALII.



Wadau wa Utalii nchini wameshauriwa kuendelea kuboresha hudama na uwekezaji katika sekta ya utalii ili kwendana na witikio chanya wa wageni nchini unaotokana na Juhudi za Serikali katika kutangaza Utalii hasa kwa kupitia Filamu ya The Royal Tour.  

Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alipokuwa akifungua mkutano wa Wadau wa Utalii wa Sekta binafsi kwa lengo kujadili kwa pamoja fursa na mapendekezo yatakayowezesha Sekta Binafsi kushiriki katika uwekezaji kwenye sekta ya utalii.


Aidha, Waziri Balozi Dkt. Chana ameendelea kumpingeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni muasisi wa Programu ya Tanzania, the Royal Tour na jitihada mbalimbali anazofanya katika kukuza na kuvutia uwekezaji wa huduma na miundombinu ya sekta ya utalii nchini.

Waziri Balozi Dkt. Chana ameongeza kuwa sanjari na maboresho mbalimbali, Wizara anayoiongoza imeanza kufanya mapitio ya Sheria ya Utalii ili kuboresha mazingira ya biashara za utalii nchini.

"Tunaendelea kushirikiana na Wizara nyingine ili kuwa na Dirisha Moja la Malipo (One Stop Shop) litakalowezesha kuwa na namba moja ya malipo (control number); kufanya kaguzi za pamoja na kuboresha sheria za kazi ili kuwatambua wapagazi na ajira za msimu". Alisema Waziri Balozi Dkt. Chana


Mkuto huo ni muendelezo wa Mkutano wa kwanza wa MPPD uliofanyika  tarehe 25 Julai, 2022  Jijini Arusha ambao pamoja na mambo mengine ulijadilili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya utalii na kutoa mapendekezo na hatua mbalimbali za kuchukua ili kuboresha mazingira ya biashara za utalii nchini.


WAZIRI BALOZI DKT. CHANA AHIMIZA UWEKEZAJI NA UBORA KWENYE SEKTA YA UTALII. WAZIRI BALOZI DKT. CHANA AHIMIZA UWEKEZAJI NA UBORA KWENYE SEKTA YA UTALII. Reviewed by Fahadi Msuya on January 07, 2023 Rating: 5