Header AD

header ads

BANDARI YA TANGA YAANZA KUHUDUMIA MELI KUBWA .



Na Hadija Bagasha Tanga, 

Bandari ya Tanga kwa mara ya kwanza imeanza kuhudumia meli kubwa kwenye gati mpya ya kisasa kwa nara ya kwanza na kuondokana na adha ya kupakua shehena kwenye meli zenye ukubwa huo umbali mrefu na kusababisha gharama kubwa za upakuaji. 

Meli hiyo yenye urefu wa mita 150 imetia nanga mapema hii leo katika bandari hiyo. 

Akizungumza wakati wa mapokezi ya meli hiyo Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha amesema meli hiyo yenye urefu wa mita 150 kutoka Nchini Urusi itaanza kuhudumiwa kwenye mradi mkubwa wa ujenzi wa gati la kisasa mradi ambao umegharimu serikali zaidi ya shilingi bilioni 429.1.


Meneja Mrisha amesema kuwa meli hiyo imeleta mzigo wa Amonium Nitrate yenye ujazo wa tani 6909.2 mzigo wa mteja kutoka Congo mzigo unaotarajiwa kupakuliwa kwa muda wa siku 2.

"Meli hii ni ya kwanza kufika hapa tangia tumekabidhiwa kipande hiki cha mita 300 ni matarajio yetu tutapata neli kubwa zaidi mradi wetu mpaka sasa unefikia asilimia 94 ambapo tarehe 4.4 2023 tutakabidhiwa mita zote 450 na hii ni dalili njema kabisa ya mafanikio ya bandari yetu, "alisistiza Meneja Mrisha. 

 Mrisha ameongeza kuwa meli hiyo imefunga gatini leo hii ni matarajio yetu baada ya watu wa afya kuja na kukagua meli hii basi tutaanza kuupakua mzigo huu kwa muda wa masaa 48 iwe imemaliza 



Amesema uwepo wa meli hiyo ni njema ya kuwa zinakuja meli kubwa zaidi kutoka duniani kote kutokana na maboresho makubwa ya kina cha bandari hiyo yaliyofanyika chini ya Rais Dkt Samia Suluhi Hassan. 

"Hii ni dalili njema sasa kwamba bandari ya Tanga dasa imefunguka ndugu waandishi naomba mtupelekee taarifa ya kwamba sasa ivi bandari ya Tanga imefunguka na tinawaahidi kwamba tutatoa huduma bora kuanzia sasa na kwa wakati, "alisema Mrisha. 

Rose Tandiko ni Mkuu wa Idara ya Masoko Bandari ya Tanga anesena hatua hiyo inatajwa kuwa ni mwanzo wa mafanikio ya bandari ya Tanga huku wafanyabiashara wakiombwa kuitumia bandari hiyo baada ya kujengewa uwezo wa kuhudumia meli kubwa za mizigo. 



Meli hiyo imekuja wakati ambao mkandarasi anayetekeleza mradi huo akiwa amekabidhi kipande cha mita 300 cha ujenzi wa gati kati ya mita 450 zinazotarajiwa kukabidhiwa mwezi April mwaka huu na kuanza kuhudumia meli kubwa za mizigo.


BANDARI YA TANGA YAANZA KUHUDUMIA MELI KUBWA . BANDARI YA TANGA YAANZA KUHUDUMIA MELI KUBWA . Reviewed by Fahadi Msuya on February 27, 2023 Rating: 5