BILIONI 5.8 ZAPELEKWA WILAYA SAME KUKARABARI BARABARA KUPITIA TARURA
OR TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Mhe. David Silinde (Mb) amesema Wilaya ya Same imetengwa kiasi cha Shilingi bilioni 5.8 sawa na asilimia 18.32 ya Bajeti ya Mkoa Kilimanjaro ya Shilingi bilioni 31.65 katika Mwaka 2022/23 kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara.
Amesema hayo tarehe 10 Februali 2023 Bugeni Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge viti Maalum, Mhe. Naghenjwa Kaboyokwa aliyetaka kujua Je, Serikali ina mpango gani wa kutenga fedha za kutosha za Ujenzi wa barabara za Wilaya ya Same baada ya kutengewa 9.5% tu ya Fedha za TARURA kwa Mwaka 2018/19.
Mhe. Silinde amesema Wilaya ya Same ina Mtandao wa Barabara zipatazo kilomita 874.64 ambazo ni sawa na asilimia 18.89 ya Mtandao wote wa Barabara katika Mkoa wa Kilimanjaro wenye kilomita 4629.45.
Amesema bajeti kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara katika Wilaya Same imekuwa ikipanda kila Mwaka wa fedha ambapo Mwaka wa Fedha 2018/19 Wilaya ya Same ilitengewa Jumla ya Shilingi bilioni 1.29
Aidha, Mhe. Silinde amesema katika mwaka wa fedha 2021/22 Wilaya ya Same ilitengewa kiasi cha Shilingi bilioni 3.7 sawa na asilimia 16.24 ya bajeti ya Mkoa ya Shilingi bilioni 22.83.
Amesema Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara katika Wilaya ya Same kadri ya upatikanaji wa fedha kwa kuzingatia mtandao wa barabara uliopo.
BILIONI 5.8 ZAPELEKWA WILAYA SAME KUKARABARI BARABARA KUPITIA TARURA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
February 11, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
February 11, 2023
Rating:

Post a Comment