Kamati ya kitaifa maboresho ya mitaala yawatembelea wataalamu kujadili maboresho katika muhtasari
Kamati ya Kitaifa ya Wataalamu inayosimamia maboresho ya mitaala ya elimu kwa Ngazi za Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu, leo tarehe 18/02/2023 imewatembelea wataalamu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Vyuo vikuu , Baraza la Mtihani Tanzania (NECTA) na Walimu wa Sekondari mjini Bagamoyo kujadiliana juu ya maboresho katika muhtasari Somo Elimu ya Biashara.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya maboresho ya Mitaala, Prof. Makenya Maboko ameongoza majadiliano hayo ambapo pia Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt. Aneth Komba , Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Educate Bwana Kamanda Kamiri, Mkurugenzi wa mafunzo ya Mitaala Dkt.Fika Mwakabungu Mkurugenzi wa Idara ya Ubunifu na uandaaji wa vifaa vya Kielimu , Bwana. Fixon Mtelesi,Mkurugenzi wa Idara ya Ubunifu na Ukuzaji wa Mitaala, Dkt.Godson Lema walihudhuria.
Kamati ya kitaifa maboresho ya mitaala yawatembelea wataalamu kujadili maboresho katika muhtasari
Reviewed by Fahadi Msuya
on
February 18, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
February 18, 2023
Rating:




Post a Comment