Header AD

header ads

bandari ya Tanga yatoa msaada hospitali ya wilaya Pangani



Na Hadija Bagasha Tanga, 

Hospitali  ya Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga inakabiliwa na uhaba wa vifaa tiba ambavyo ni muhimu kwajili ya kuwasaidia wagonjwa wanapoenda kupata matibabu.

Zoezi la kugawa vifaa tiba vikiwemo vitanda na magodoro limefanyika kwenye hospital ya wilaya ya Pangani kwajili ya kuwasaidia wagojwa.

Bandari ya Tanga imetoa msaada huo wenye thamani ya zaidi milioni 31 lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto iliyokuwa inakabiliana hospital hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo  Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha amesema kuwa msaada waliotoa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii kile walichokipata. 


"Mamlaka ya usimamizi wa bandari katika kutekeleza shughuli zake imepata hicho kilichopatikana katika mahesabu yake sasa tunakitoa kwa maana ya kurudisha katika jamii tunakitoa kile tulichopata cha mwaka 2021/22 tunakirudisha sasa katika jamii, alisisitiza Meneja Mrisha. 


Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Issaya Mbenje amesema kwa kiasi kikubwa msaada huo wa vitanda 15 na magodoro vinakwenda kutufanya wawe na uwezo wa kulaza wagonjwa wengi zaidi ya idadi waliyokiwa wakihudumia. 


"Hii itasaidia kwani vitanda vingine vilikuwa vimeshaanza kuchoka vimechakaa sasa vile vinaondolewa maana yake tunapata vitanda vipya na magodoro mapya, "alibainisha Mmbenje

Kwa upande wake Kaimu mganga mkuu wa wilaya hiyo DKT Hassan Msafiri amesema kiwa vifaa hivyo itasaidia kukabiliana na changamoto iliyokuwepo.

"Kwetu ni msaada mkubwa sana kwasababu unakwenda kuongeza uwezo wa hospitali yetu ya wilaya ya Pangani ambayo kwa siku tulikuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 50 mpaka 60 lakini kupitia msaada huu tunakwenda kuongeza uwezo na kwenda mpaka wagonjwa 75,"alisema Kaimu Mganga huyo. 


Msaada huo umekuja wakati hospital ikiwa kwenye ukarabati ambao unaighalimu serikali kiasi Cha  shilingi milioni mia tisa.



bandari ya Tanga yatoa msaada hospitali ya wilaya Pangani bandari ya Tanga yatoa msaada hospitali ya wilaya Pangani Reviewed by Fahadi Msuya on July 21, 2023 Rating: 5