Kituo cha Sayansi kujengwa Jijini Dodoma
Na Hadija Bagasha Tanga,
Waziri wa Elimu Sayansi na teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema Serikali kwa kushirikiana na Project Insipire ipo kwenye mchakato wa kujenga kituo kikubwa cha Sayansi na teknolojia Mkoani Dodoma ambacho kitatumiwa na viongozi wengine wa serikali kama mfano utakaosaidia vituo vya aina hiyo kujengwa maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi.
Profesa Mkenda ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea kituo cha sayansi cha Stem park kilichopo jijini Tanga, mpango ambao amesema utasaidia kumaliza tatizo la wanafunzi kutopenda masomo ya sayansi.
Waziri Mkenda amesema kituo ambacho kitajengwa mjini Dodoma kitakuwa kama kituo cha mfano ambacho wabunge na viongozi wengine wa serikali watakitembelea ili kuona umuhimu wa kuwa na vituo vya aina hiyo kwenye maeneo yao.
"Dodoma ni katikati ya nchi yetu halafu pale wabunge, mawaziri wenzangu na watu mbalimbali wakuu wa mikoa nitapenda watembelee pale waone nini kinaweza kufanyika vituo hivi vinapaswa kujengwa kila mikoa najua haitafikia wanafunzi wote vitu vyote hivi ni matumda ambayo yanapatikana kkirahisi, "alisema Waziri Mkenda.
"Kwahiyo mimi mwenyewe nitasapoti kwanza tutafute eneo jiji la la Dodoma litupe eneo litupe na majengo waje pale na tusiwatoze hata thumni kwasababu wenyewe hawawatozi wanafunzi wanaokuja kufanya mafunzo hapa hawalipishwi chochote,"alisisitiza Prof Mkenda.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Project insipire Lwidiko Edward amesema kituo hicho kinawatengeneza wanafunzi kwenye masomo ya sayansi kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo kujifunza kwa miradi na kuandaa mazingira yanayotoa hamasa ya kusoma.
Mkurugenzi mkuu wa tume ya sayansi na teknolojia Costech Amos Nungu amesema kituo hicho kitasaidia kujenga mapenzi ya watoto kupenda masomo ya sayansi tokea wakiwa katika umri mdogo.
Mpango wa ujenzi wa vituo hivyo unakuja wakati kukiwa na ari ndogo ya wanafunzi wanaopenda masomo ya sayansi ambao wengi wamekuwa wakikimbilia masomo ya sanaa kutokana na mazingira duni ya kujifunza masomo hayo.
Kituo cha Sayansi kujengwa Jijini Dodoma
Reviewed by Fahadi Msuya
on
July 11, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
July 11, 2023
Rating:





Post a Comment