Header AD

header ads

MBUNGE TARIMBA AMWAGIA SIFA RAIS SAMIA,BAADA YA KUFANYA JAMBO HILI.



MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni,Abbas Tarimba,amempongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassani,kwa kutoa milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya kilichopo Kata ya Kinondoni .

Tarimba ametoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akifanya ziara ya kuangalia maendeleo ya hospitali hiyo ambayo imeanza kutoa huduma.


"Natoa pongezi sana kwa Rais Samia kwa kutoa fedha hii ni kwa mara toka kata hii ianzishwe kuwa na kituo cha Afya"Amesema Tarimba.

Hata hivyo Tarimba amewataka wananchi kujitokeza kujipatia huduma katika hospitali na kubainisha kuwa huduma zinazotolewa hapo ni za kisasa na bora,

Sanjari na hayo,Tarimba ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya mchezo wa kubashiri wa Sport Pesa,amehaidi kujenga kisima cha kisasa cha maji.

"Natoa ahadi hapa nikimtaka mganga anioneshe eneo nzuri ili niweze kujenga kisima cha kisasa"Ametoa Ahadi Tarimba.

Awali akizungumzia Hospitali hiyo,Mganga mkuu wa Hospitali,Dkt Juliasi Nyakazilibe,amewataka wananchi kujitokeza kujipatia huduma katika hospitali hiyo kwakuwa ni za kisasa.

Dkt Nyakazilibe,amesema kwa sasa wanachangamoto ya uhaba wa watumishi huku akisema watumishi waliopo ni wachache jambo lilomfanya kujibiwa na Mbunge Tarimba kusema teyari suala hilo ameshalifikisha Bungeni na teyari watumishi wanatarajiwa kuwasili.
MBUNGE TARIMBA AMWAGIA SIFA RAIS SAMIA,BAADA YA KUFANYA JAMBO HILI. MBUNGE TARIMBA AMWAGIA SIFA RAIS SAMIA,BAADA YA KUFANYA JAMBO HILI. Reviewed by Fahadi Msuya on July 25, 2023 Rating: 5