Header AD

header ads

Serikali yaendelea na ujenzi wa veta 65 nchini



Na Hadija Bagasha Tanga, 

Serikali imesema inaendelea na ujenzi wa vyuo 65 vya ufundi stadi Veta katika Mikoa na Wilaya mbalimbali nchini ikiwa ni mkakati wa serikali katika kuhakikisha inatoa elimu ya amali ambayo inakidhi matakwa na kutoa huduma mbalimbali. 

Waziri Mkenda ameyasema hayo alipotembelea chuo cha ufundi stadi Veta jijini Tanga ili kujionea namna kinavyotoa mafunzo ya ufundi stadi lakini pia kuhakikisha wanatoa huduma zinazostahiki. 


Waziri Mkenda amesema kuwa kati ya vyuo 65 vinavyojengwa vyuo 64 za Wilaya na moja ya Mkoa huku matumaini yakiwa makubwa katika kila maeneo yanayojengwa vyuo hivyo. 

"Tukiwa bungeni swali kubwa ambalo limekuwa likiulizwa mara nyingi kuliko maswali mengine yote katika wizara ya elimu sayansi na teknolojia ni kuhusu veta kila mmoja anauliza ni lini veta itajengwa kwake watu wanatarajio makubwa sana kwenye veta kwa maana hiyo sisi tuna kazi ya kuhakikisha tunakidhi matarajio yao kwa kutoa elimu ya amali ambayo ni bora na ambayo inakidhi matakwa, "alisema Waziri Mkenda. 


Alisema zipo namna mbili za kuendelea kujipima ambapo moja ni kuangalia wahitimu wanafanya wapi kazi mara baada ya kuhitimu mafunzo yao na kuwahoji waliowaajiri namna kuwa wanaridhika kwa namna gani na utendajo wao. 

Antony Kasore Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi Veta amesema watahakikisha wanakwenda kutekeleza maagizo ya Waziri ya utoaji wa mafunzo bora na kuhakikisha wanatoa mafunzo yanayohitajika na yanayozingatia ubora bao unahitajika. 



"Kama tulivyosikia kuna vyuo vinavyojengwa 65 katika wilaya mbalimbali na Mkoa na chenyewe pia tunakwends kusimamia kama maelekezo aliyotoa ya kuhakikisha tunasimamia ujenzi huo uweze kufanyika tukiamini tutakuwa tumekwenda kutekeleza yale yote yaliyoanishwa, "alisema 


Serikali yaendelea na ujenzi wa veta 65 nchini Serikali yaendelea na ujenzi wa veta 65 nchini Reviewed by Fahadi Msuya on July 12, 2023 Rating: 5