TIKETI ZA MTANDAO ZAJA,WATANZANIA WANATAKIWA KUZITUMIA.
KAMPUNI ya Global Light and Company Limited imezindua mfumo wa ukatiaji tiketi za kielektroniki kwamagari ya kukosa (Tiketi Rafiki Special Hire).
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo leo Julai 13, 2023 Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Richard Simon amesema Tiketi Rafiki ni moja ya mfumo wa utoaji tiketi za kielektroniki kwa wasafiri waendao mikoani na wilayani katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
“Mifumo ya utoaji tiketi za kielektroniki ipo chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA). Hivyo basi kwa mantiki hiyo, Tiketi Rafiki hifanya Kazi ya kuhudumia abiria chini ya miongozo ya LATRA,” amesema Simon.
Kwamba mfumo huo uliundwa ili kukidhi hitaji la utoaji tiketi za kielektroniki kwa abiria wanaohudumiwa na watoa Huduma ya usafirishaji abiria kwa magari ya kukodi.
Simon amesema mfumo huo umezingatia mahitaji ya watoa huduma wa magari ya kukodi ambayo ni tofauti kabisa na mahitaji ya watoa ya huduma ya isafiri wa Mabasi yaendayo mikoani na wilayani.
“Hivyo basi kutofautiana kwa mahitaji ya watoa huduma ya Usafiri, Tiketi Rafiki Special Hire ni Maalum kwa watoa huduma wa magari ya kukodi hasa Mabasi madogo yanayosafirisha abiria Wenye lengo Maalum,” ameongeza Simon.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Raymond Magambe akitaja faida za mfumo huo amesema ni pamoja na kukidhi takwa la koshiria la usafirishaji kwa wasafirishaji kuwa na mfumo wa utoaji tiketi za kielektroniki,”.
Nyingine ni kusaidia ni kusaidia kupaa Takwimu za wasafiri wanaotumia magari ya kokodi mara zinapojitajika katika mipango ya maendeleo ya Serikali.
Vile vile mfumo huo husaidia mmiliki wa chombo cha Usafiri kukata taarifa za muamala kwa safari mbalimbali zinazofanyika au zikizokwisha fanyika,”ammagambe.
Kwamba mfumo huo utasaidia mmiliki wa Chombo cha Usafiri kupata kumbukumbu za Biashara mara atakapo zihitaji.
Amebainisha kwamba ili mtoa huduma ya Usafiri wa magari ya kokodi aweze kuunganishwa na mfumo wa Tiketi Rafiki.
TIKETI ZA MTANDAO ZAJA,WATANZANIA WANATAKIWA KUZITUMIA.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
July 15, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
July 15, 2023
Rating:

Post a Comment