Header AD

header ads

WANANCHI WAJIVUNIA UWEPO WA VYUO VYA MALIASILI NA UTALII, 77.



Na Sixmund J. Begashe

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi ya  Wanyamapori Pasiansi imepongezwa  kwa Mafunzo na program mbalimbali inazoendesha kwa lengo la Usimamizi wa Wanyamapori na Hima Sheria. 

Wakipita kwenye Banda la Maliasili na Utalii lililopo kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) Jijini Dar es Salaam, wananchi wengi wamevutiwa na uwepo wa Chuo hicho ambacho kinatoa mchango mkubwa nchini katika Uhifadhi na ulinzi wa Raslimali za Taifa.


Bw. Chance Enock ambaye ni Mkazi wa Chalinze, amesema, Mafunzo yanayotolewa na Chuo hicho, yanaendelea kuwa muhimili katika ulinzi wa Wanyamapori, katika maeneo  yaliohifadhiwa kisheria pamoja na wananchi wanaoishi pembezoni mwa Hifadhi za Taifa. 

"Mwenyezi Mungu katujalia raslimali lukuki, kama si mikakati ya Serikali yetu ya kuwa na Chuo hiki na vinginevyo kunoa vijana wakuilinda, sisi tusinge nufaika nayo na tungekosa kitu cha kurithisha watoto wetu, kwa kweli nimeelimika na ujio wangu hapa 77 ,". Alisema Bw. Enock

Akizungumzia chuo hicho kilichopo Mkoani Mwanza, Makamu Mkuu wa Chuo Mafunzo, Utafiti na Ushauri elekezi, Bi. Ester Mtamenywa- amesema Chuo  kinatoa ujuzi wa kozi za Usimamizi wa Wanyamapori na Hima Sheria, Kuongoza Wageni , na Usalama wa Wageni. Pia Chuo  kinaendesha Kampuni ya Ulinzi - Pasiansi Security Company( PASCO)ambayo inatoa huduma kwenye maeneo yaliyo hifadhiwa, ametoa wito Kwa wananchi na wadau mbalimbali kushirikiana na chuo hicho kwa maslahi mapana ya nchi.


WANANCHI WAJIVUNIA UWEPO WA VYUO VYA MALIASILI NA UTALII, 77. WANANCHI WAJIVUNIA UWEPO WA VYUO VYA MALIASILI NA UTALII, 77. Reviewed by Fahadi Msuya on July 12, 2023 Rating: 5