Header AD

header ads

CCM Tanga yapongeza wizara ya maji



Na Hadija Bagasha Tanga, 

Wakazi wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga wameanza kupata maji safi kwa asilimia kubwa kufuatia kukamilika kwa mradi wa maji wa shililingi bilioni 6 ambao unatokana na chanzo cha maji cha mto zigi. 

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm Mkoa Tanga Rajab Abrahaman Abdalah ameishukuru serikali kupitia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia tatizo hilo la muda mrefu la ukosefu wa huduma ya maji lililokuwa likiwakabili wakazi wa wilaya hiyo. 

"Chama cha mapinduzi ccm Mkoa Tanga kinamshukuru sana mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kiukweli anatuondolea kero ya maji katika vijiji karibu vyote kwenye Mkoa wetu wa Tanga kwenye kata zote,  kwenye miji yetu mheshimiwa Rais anatupatia fedha nyingi sana, "alisema



"Changamoto hii ya maji haiwezi kumalizika kwa wakati mmoja lakini ukiangalia huko miaka ya nyuma na sasa kiukweli ni tofauti vipo vijiji tunavijua kabisa kama kule kwetu Pangani kuna kijiji cha mtango watu walikuwa wanatembea kilomita 7 kwenda na kurudi kwajili ya kutafuta ndoo moja tu ya maji, maana yake alikuwa anatembelea kilomita 14 au 15 lakini sasa adha hiyo imepungua kwa kiasi kikubwa, "alisisitiza Mwenyekiti Rajab. 

Mwenyekiti Rajab amesema chama hicho kinampongeza Rais Dkt Samia,  Waziri wa maji Jumaa Aweso pamoja na timu yake nzima ya wizara ya maji,  na Ruwasa kwa kazi kubwa na nzuri ambazo wamekuwa wakizifanya Mkoani Tanga. 


"Tunawapongeza sana Ruwasa kwa kushirikiana na Waziri wa maji kwenye mkoa mzima wa Tanga mmekuwa mkifanya kazi kubwa sana ya kutuondolea adha ya maji kwenye vijiji vyetu changamoto hizi huwa hazimaliziki kwa mara moja lakini zile sehemu tunazobanana tunafanya hivyo ili kusukuma mambo yaende lakini tunawapongeza sana ndugu zetu wote niliowataja bila kuwasahau Tanga Uwasa, "alisema Rajab.

Aidha Mwenyekiti Rajab ametoa wito kwa wale wote wanaofanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji ikiwemo kufanya shughuli za kilimo,  uchimbaji wa madini na ukataji wa miti hovyo kuacha mara moja tabia hiyo ili kuendelea kuvilinda vyanzo hivyo. 

Meneja wa maji kutoka mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tanga Uwasa wilaya ya Muheza Ramadhani Nyambuka amesema kuwa mahitaji ya maji katika mji wa Muheza ni mita za ujazo 5500 ambapo hivi sasa kinachopatikana ni mita za ujazo  3400.

Baadhi ya wananchi waliozungumza kuhusiana na huduma hiyo ya upatikanaji wa maji kayika mji wa Muheza wamesema kwa sasa wana nafuu kubwa ukilinganisha na hapo awali. 

Tatizo la maji katika wilaya hiyo linatarajiwa kuisha kabisa kufuatia mradi mwingine wa maji ambao utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 40 ukihusisha miji minne ikiwemo  Wilaya ya Muheza,  Pangani,  Korogwe na Handeni. 


CCM Tanga yapongeza wizara ya maji CCM Tanga yapongeza wizara ya maji Reviewed by Fahadi Msuya on August 03, 2023 Rating: 5