SAKATA LA UWEKEZAJI BANDARINI,LAWAIBUA WANASHERI KUMI.
Jopo la wanasheria kumi wa kujitegemea likiongozwa na Mwanasheria Juma Nassoro, linatazamia kuiomba mahakama kuwaruhusu kuendesha kesi binafsi au kumuamuru DPP kuwafungulia mashtaka watu wanaotumia lugha za matusi na ubaguzi katika mijadala hukusu Makubaliano Kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uendeshwaji wa bandari ya Dar es Salaam,
Hayo yamebanishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwanasheria wa Kujitegemea Salim Aboubakar, wakati akizungumza kuhusu maeneo mbalimbali ya makubaliano baina ya nchi hizo mbili katika usirikiano wa bandari, ambapo wamesema uamuzi huo wataufanya kutokana na uzalendo na taifa lao.
Akizungumza kuhusu Makubaliano hayo, Mwanasheria wa kujitegemea Yahya Njama, amewataka watu wote kuacha kuingiza siasa na ubaguzi wa aina yoyote katika suala hilo, na kuwataka kuwasilisha hoja mbadala pindi wanadhani uwekezaji huo hauna manufaa kwa taifa.
Kwa upande wake, Mwamasheria Juma Nassoro amesema DP World ambayo ndio kamouni itakayotekeleza meneo ya makubaliano hayo, imeendesha bandari zaidi ya 70 duniani kwa mafanikio na hakuna mgogoro wowote wa Kidiplomasia kati ya Dubai na UAE katika uendeshaji wa Bandari hizo kama ambavyo itakuja kuendesha bandari ya Dar es Salaam.
SAKATA LA UWEKEZAJI BANDARINI,LAWAIBUA WANASHERI KUMI.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
August 05, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
August 05, 2023
Rating:

Post a Comment