Header AD

header ads

CHALAMILA AITAKA LATRA KUONGEZA KASI KIDIJITALI




NA MOSES MWAKIBOLWA

MKUU wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albart Chalamila ameitaka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini - LATRA kuhakikisha inaweka utaratibu mzuri wa utunzaji wa kumbukumbu ili kupatikana uwiano baina ya watoa huduma za usafiri na wananchi ili kuongeza kasi ya Maendeleo na kuunga mkono Jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya Dokta Samia Suluhu Hassan


Ameyasema hayo leo Jijini Dar Es salaam wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau wa usafiri na LATRA kilichofanyika katika ukumbi wa Anautoglou na kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kufanya kazi kisasa ili kuepusha malalamiko kutoka kwa abiria, kuepuka kuongeza nauli kiholela bila kufuata sheria


Chalamila ameitaka LATRA kuhakikisha inaweka kanzidata ili kuongeza ukisasa na ameongeza kuwa uwekaji wa kumbukumbu utasaidia kujua mahitaji halisi ya huduma ya vyombo vya usafiri ili kuweza kubaini ni wateja wangapi watahitaji huduma na kusaidia uwekaji wa kumbukumbu za mapato hasa kwa wale wanaohitaji mikopo au kujitathmini katika utendaji 

Naye mkurugenzi mkuu wa LATRA Habibu Suluhu amewataka madereva na makondakta kufuata sheria zilizopo pindi wanapokuwa kwenye shughuli zao za kila siku ili kuongeza ufanisi wa kazi zao na kuepuka lawama za mara kwa mara kutoka kwa abiria

Mkurugenzi huyo amesema uwepo wa kikao hicho kina umuhimu mkubwa kwa wadau kuwasilisha maoni ya ongezeko la nauli ili waweze kusikilizwa, Suluhu amesema kifungu cha 21 cha sheria za LATRA ikisoma Pamoja na kanuni ya 9.3 ambayo inazungumzia marejeo ya uwekezaji (return of investment) inayataka makampuni ya usafirishaji kurudi LATRA kuwasilisha maoni iliwaweze kusikilizwa na wadau wa usafi waweze kutoa maoni
 “Maoni ni lazima yazingatie tathmini ya kiuchumi kwa watanzania, ili kuendana na kasi ya maendeleo na kuongeza nafuu ya Maisha, pia usafiri ni kitu muhimu sana kwa kila binadamu ili kuweza kukidhi mahitaji ya kila siku, hivyo basi kila mmoja azingatie weredi katika utoaji maoni kuzingatia mahitaji ya wananchi” alisema
CHALAMILA AITAKA LATRA KUONGEZA KASI KIDIJITALI CHALAMILA AITAKA LATRA KUONGEZA KASI KIDIJITALI Reviewed by Fahadi Msuya on October 19, 2023 Rating: 5