Header AD

header ads

CP WAKULYAMBA ATAKA WOTE WALIOPORA SILA NA KUJERUI ASKARI WA JU WATIWE NGUVUNI.




Na Sixmund Begashe

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Kamishna Benedict Wakulyamba ameliagiza Jeshi la Uhifadhi (JU),kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya ulinzi na Usalama kuhakikisha wote waliohusika na tukio la kupora silaha na kujeruhi askari wa jeshi hilo walilokuwa wakaitekeleza majuakumu yao katika Msitu wa Hifadhi Irangi wakamatwe Maramoja.

Kamishna Wakulyamba ametoa agiza hilo Wilayani Kondoa alipowatembelea askari waliojeruhiwa  kwa kushambuliwa na wanavijiji zaidi ya miamoja, wa kijiji cha Mafai, pia kufanya kikao na  Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kondoa ili kupata uwelewa wa pamoja wa kukomesha huo uwalifu na mashirikiano zaidi katika uhifadhi wa Maliasili.


Ameongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inasisitiza amani, maelewano na mshikamano wa kitaifa, hivyo nivyema wananchi wakaiunga mkono kwa kuachana na vitendo vya uvunjifu wa amani, na kuwa kwa yeyote anayejaribu kuvunja amani kwa kulijaribu  Jeshi la Uhifadhi  hawata vumiliwa kamwe. 

Aidha Kamishna Wakulyamba amelaani vikali tukio hilo la kinyama lililofanywa na wananchi hao wachache wa Kijiji cha  Mafai Wilayani Kondoa, na kusema Wizara hiyo haitavumilia kamwe uovu huo na kuwa wote waliohusika nilazima wakamatwe.


Kamishna Wakulyamba ameushukuru uongozi wa Wilaya hiyo kwa hatua za haraka ulizozichukuwa kupitia vyombo vya ulinzi na usalama kushirikiana na Jeshi la Uhifadhi na katika changamoto iliyotokea na  kuhakikisha  silaa iliyoporwa inapatikana na pia kwa uongozi wa Hospitali ya Kondoa mjini kuwahudumia vyema askari waliojeruhiwa.

Naye Askari Muhifadhi daraja la tatu Hassani Yewa, akiwa amelazwa katika Hospital ya Kondoa Mjini, ameushukuru uongozi wa Wizara kwa kuungana nao katika maumivu aliyonayo na kaongeza kuwa hiyo imemtia moyo yeye na Watumishi wengine wa kufanya kazi kwa bidii na hasa pindi atakapo rejea katika majukumu yake.


Akizungumzia hali ya majerui waliolazwa hospitalini hapo, Muuguzi Bi Gema Kilumanga, amesema hali yao kwa sasa zinaendelea vyema, na wanaendelea kumpatia matibabu zaidi Martenus Mahoka na kuwa naye anaendelea vizuri.

Awali akitoaka Taarifa ya tukio hilo, Mhifadhi Misitu wa Wakala wa Misitu Tanzania wa Wilayani Kondoa Kasuka Ngunila, ameeleza kuwa wanakijiji wa Mafai zaidi ya miamoja, waliwavamia askari wa Jeshi la Uhifadhi na kuwajerui huku wakipora silaha, baada ya kukamata mifugo zaidi ya 138 ndani ya Msitu wa  Hifadhi Irangi, Wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma.
CP WAKULYAMBA ATAKA WOTE WALIOPORA SILA NA KUJERUI ASKARI WA JU WATIWE NGUVUNI. CP WAKULYAMBA ATAKA WOTE WALIOPORA SILA NA KUJERUI ASKARI WA JU WATIWE NGUVUNI. Reviewed by Fahadi Msuya on October 10, 2023 Rating: 5