Header AD

header ads

CWT MAGU YAANZA MAANDALIZI BONANZA LA MIAKA 30 YA CWT TAIFA , YAAHIDI USHINDI




Kuelekea maadhimisho ya miaka 30 ya Chama cha Walimu Tanzania CWT  na siku ya Mwalimu duniani Novemba 4, 2023  Mkoani Mwanza ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan , Chama cha Walimu Wilayani Magu kimeanza rasmi maandilizi ya kutafuta timu kwaajili ya kushiriki bonanza litakalohusisha michezo mbalimbali siku ya maadhimisho hayo.

Akizungumza wakati wa bonanza kwaajili ya kutafuta timu ya walimu itakayoshiriki michuano hiyo Mweka hazina wa CWT Wilayani Magu Mwalimu Ruhumbika Kapesa amesema lengo la kufanya maandalizi hayo kupata timu ya ushindani ambayo itaenda kushindana na kurudi na ushindi .



" Tumejiandaa vizuri kwaajili ya bonanza hilo na lengo letu ni kuwa na timu ya Walimu Wilaya ya Magu ambayo itakuwepo kwa muda wote na si kukaa na kusubiri mashindano yatokee ili tuanze kutafuta timu hivyo tunatarajia kusajili timu hii ili kuhamasisha walimu kushiriki katika michezo" amesema 

Ameongeza kuwa " tunataka timu yetu ianze kutoka nje ya Wilaya kushiriki michezo katika ngazi ya Mkoa na kitaifa ili kufanikisha zoezi la kuwaunganisha walimu kwa pamoja kupitia michezo"

Kwa upande wake Mchezaji wa timu ya CWT Magu ,  Mwalimu Anderson Kidai amesema wao kama wachezaji wamejiandaa kufanya vizuri na walimu wengi wamejitokeza na wanaonesha juhudi za kutaka kupata nafasi ya kuwakilisha timu ya Walimu Magu katika bonanza la siku ya Mwalimu duniani Mkoani Mwanza.


Naye kocha wa timu  Mwalimu Nicholaus Molel amesema wachezaji wana ari nzuri na kubainisha kuwa atapata timu imara ambayo itawakilisha vyema Wilaya ya Magu katika Bonanza hilo.

Akizungumzia maandalizi ya timu ya ' NetBall ' Mwalimu Balbina Kiza amesema wamejipanga kupata ushindi wa kishindo kwa upande wa wanawake na kubainisha kuwa mwitikio wa walimu katika maandalizi ni mkubwa na kuridhisha.

Amesema timu hiyo itakua endelevu na wataendelea kushiriki katika mashindano mbalimbali  ili kufikia malengo ya  kuitangaza CWT kwa njia ya michezo .


CWT MAGU YAANZA MAANDALIZI BONANZA LA MIAKA 30 YA CWT TAIFA , YAAHIDI USHINDI CWT MAGU YAANZA MAANDALIZI BONANZA LA MIAKA 30 YA CWT TAIFA , YAAHIDI USHINDI Reviewed by Fahadi Msuya on October 07, 2023 Rating: 5