MAKAMU WA PILI WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ATOA TAMKO KWA WANASIASA UCHAGUZI 2025.
Na Hadija Bagasha Pangani,
MAKAMU wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapindunzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla na mlezi wa CCM Mkoa wa Tanga amesema wanasiasa wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao maeneo yao ya utawala waanze kujiandaa kuachia nafasi zao kwa kuwa chama hicho kinahitaji kuingia na watu wanaouzika kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.
Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla anaitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanachama wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Pangani na Muheza akiwa kwenye ziara yake ya kichama kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
"Ambaye anahisi hawezi kukamilisha maono hayo basi njoo umnong'oneze Mwenyekiti wa Wilaya mapema kama unaona roho yako nzito nzito kidogo hutaweza kukamilisha hili muarifu kabisa mwenyekiti wa ccm Wilaya, muarifu kavisa kamisaa wa wilaya ili wewe tukuweke pembeni, "alisistiza Makamu wa pili.
Amesema kwa kufanya hivyo kutakisaidia chama kupata kiongozi mzuri atakayeweza kuwatumikia wananchi na kukipa ushindi chama hicho.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tanga,Rajabu Abdalah amesema nidhamu kwa watumishi imeanza kuimarika hususani kwenye usimamizi wa mirasdi ya maendeleo huku mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumzia ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi ujao.
"Yapo mambo ambayo yamekuwa nje ya uwezo wa Mkuu Mkoa nikawasiliana na wewe na wewe ukawasiliana na mamlaka husika zimeweza kuchukuliwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania na sasa nidhamu ya watumishi waserikali na waliopewa dhamana ya kusimamia miradi ya serikali kwenye Mkoa wetu wa Tanga angalau sasa imeanza kutengamaa, "alisisitiza Mwenyekiti Rajab.
"Lakini pia niseme kwa kinywa kipana kama nilivyosema kwenye maeneo mengine tuliyopita kwamba wote ambao Rais ameleta fedha za miradi mbalimbali badala ya kutekeleza miradi hiyo wamekula fedha za serikali kiukweli sisi katika Mkoa wa Tanga hatuwezi kukubali fedha zile watazitapika kwa njia yeyote ile, "alisema Rajab.
Mkuu wa Mkoa Waziri Kindamba amemuhakikishia Makamu wa pili wa Rais kuwa tayari Rais ameshinda katika uchaguzi mkuu ujao na hiyo ni kutokana na maendeleo makubwa aliyoyafanya kwa Watanzania.
"Tayari Dokta Samia Suluhu Hassan hapa Pangani ameshinda tunachokitafuta sasa ni ule ushindi wa kishindo na mimi nikuhakikishie ushindi huo wa kishindo hapa Pangani utapatikana, "alibainisha Kindamba.
Makamu wa pili wa seriakali ya mapinduzi ya Zanziba amekutana na wanachama wa chama hicho katika wilaya ya Mkinga, Pangani na baadae atakutana na wanachama wa chama hicho katika wilaya ya Kilindi ,Handeni na kasha wilaya ya Lushoto na wilaya ya Korogwe.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ATOA TAMKO KWA WANASIASA UCHAGUZI 2025.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 11, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 11, 2023
Rating:





Post a Comment