Header AD

header ads

NBAA YAZINDUA VIWANGO VYA MAENDELEO ENDELEVU ILI KUISAIDIA SERIKALI KUTIMIZA LENGO LA SDG 2023

Msaidizi Muhasibu Mkuu wa Serikali CPA Azizi Kifile akizungumza wakati wa uzinduzi wa Viwango Vipya vya Hesabu vya Kimataifa vya Maendeleo Endelevu yenye lengo la kusaidia serikali katika juhudi za kufikia malengo ya maendeleo endelevu 2030 (SDG 2030) uliofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia Temu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Viwango Vipya vya Hesabu vya Kimataifa vya Maendeleo Endelevu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno akziungumza kuhusu namna walivyojipanga kuweza kusimamia Viwango Vipya vya Hesabu vya kimataifa vya Kuripoti Maendeleo Endelevu na jinsi NBAA itakavyosaidia Taasisi mbalimbali katika kufikia malengo hasa kwenye kutumia viwango hivyo.

Mjumbe wa Bodi ya Kimataifa ya mahesabu kwa Sekta ya Umma (IPSASB), CPA Dkt Neema Kiure akiwasilisha mada kwa wadau mbalimbali waloudhuria uzinduzi wa Viwango Vipya vya Hesabu vya Kimataifa vya Maendeleo Endelevu.

Mgeni Rasmi Msaidizi Muhasibu Mkuu wa Serikali CPA Azizi Kifile (kushoto) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Viwango Vipya vya Hesabu vya Kimataifa vya Maendeleo Endelevu yenye lengo la kusaidia serikali katika juhudi za kufikia malengo ya maendeleo endelevu 2030 (SDG 2030). Viwango hivyo ni Uwazi katika kuripoti maendeleo endelevu (IFRS S1) na Uwazi katika kuripoti athari za kwenye mazingira (IFRS S2) vitakavyotumiwa na Taasisi zote nchini Tanzania za Umma na Binafsi kuanzia Januari 01, 2024, Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia Temu na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius A. Maneno.

Mgeni Rasmi Msaidizi Muhasibu Mkuu wa Serikali CPA Azizi Kifile  akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia Temu, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno, Wafanyakazi wa Bodi hiyo pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Viwango vya kimataifa vya Maendeleo Endelevu uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam.
NBAA YAZINDUA VIWANGO VYA MAENDELEO ENDELEVU ILI KUISAIDIA SERIKALI KUTIMIZA LENGO LA SDG 2023 NBAA YAZINDUA VIWANGO VYA MAENDELEO ENDELEVU ILI KUISAIDIA SERIKALI KUTIMIZA LENGO LA SDG 2023 Reviewed by Fahadi Msuya on October 19, 2023 Rating: 5