Header AD

header ads

Ofisi ya wakili mkuu wa serikali yaokoa mabilioni ya fedha.




Na Hadija Bagasha Tanga, 

OFISI ya wakili mkuu wa serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 imeendesha jumla ya mashauri 7, 392  huku ikifanikuwa kuokoa kiasi cha shilingi Billion 609, 368, , 184, 378.32 pamoja na Dola za kimarekeni Million  37, 341, 177 fedha ambazo zingelipwa  na wadaiwa endapo serikali ingeshindwa kwenye mashauri hayo.

Hayo yamebainishwa mkoani Tanga na  mwenyekiti wa baraza  na wakili  mkuu wa serikali Dkt. Boniface Luhende  wakati akifungua  kikao cha kwanza cha baraza la pili la wafanyakazi wa ofisi ya wakili mkuu wa serikali  kwa mwaka wa fedha 2023/2024  ambapo amesema kati ya mashauri hayo 7, 255 ni ya madai na 137 ni ya usuluhishi.


Dkt Luhende amesema kati ya mashauri hayo 7350 ni ya ndani na 41 ni ya nje  huku ofisi hiyo ikiwa imefanikiwa kumaliza jumla ya mashauri 620, 579 yakiwa yamemalizika kwa njia za kimahakama   41 yakimalizika ni  kwa njia ya majadiliano ya nje ya mahakama.

Katika kuendelea kutekeleza majukumu ya ofisi hiyo   kwa maslahi mapana ya Taifa   Dkt Luhende amewaasa watumiahi wote waliopo katika vitengo mbalimbali kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumj yao ipasavyo kwa kuzingatia sheria,   uzalendo uandilifu , na kudumisha ushirikiano.



" Nitoe rai kwenu wajumbe na mfikishe salam hizi wa watumishi  wengine  kuwa tushirikiane kikamilifu  tukizingatia  uzalendo uandilifu umoja na mshikamano  bila kusahau sheria  taratibu na kanuni za utumishi wa umma katika  kutekeleza  vyema majukumu yetu kuendana na bajeti tuliyopatiwa na dhamana tuliyokasimiwa " alisisitiza Dkt Luhende. 

Aidha ameeleza kuwa ofisi ya wakili mkuu wa serikali  imefanikiwa na inaendelea kutatua migogoro mbalimbali nje ya mahakama ili kuzidi kuwavutia wawekezaji na wafanyabishara kupitia sekta ya sheria.

 "Ili kutambua  mchango wa wawekezaji ,  wafanyabishara pamoja na wawekezaji ofisi imesuluhisha migogoro mbalimbali  kwa njia ya majadiliano  nje ya mahakama  na mabaraza  hatua ambayo imesaidia kukuza imani ya wawekezaji na wafanyabiashara  kwa sekta ya sheria  nchini pia imekuwa moja ya vivutio  kwa wawekezaji nchini" alisema.



Ameongeza kuwa ofisi wa wakili mkuu wa serikali inaendelea kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa  katika maadhimisho ya wiki ya sheiria nchini ambapo aliwataka kushughulikia notisi za siku 90 zilizotolewa dhidi ya serikali ili kupunguza  idadi ya mashauri na kuimarisha utatuzi wa migogoro kabla ya kuwasilishwa  mahakamani  ambapo katika kutekeleza hilo tayari  kwa kipindi cha mwezi january hadi june 2023 tayari notisi 333 zimeshashughulikiwa.

Awali akizungumza makamu mwenyekiti wa baraza hilo kutoka ofisi ya wakili mkuu wa serikali Mark Mulwambo amesema kuwa ili kuboresha utendaji na ufanisi wa majukumu yao  kwa mwaka wa fedha 2023/2024 wamedhamiria kuhakikisha kuwa wanawajengea uwezo kwa kuwapa mafunzo ya kiutendaji watumishi  wote pamoja na kuimarisha mifumo ya Tehema nchini.



"Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ofisi ya wakili mkuu wa serikali imejiwekea bipaumbele mbalimbali ikiwemo kuwajengea uwezo watumishi kwa kuwapa magunzo ya muda mrefu na muda mfupi ya kibobevu katika maeneo maalumu kama sekta ya mafuta na gesi na kuendelea kuimarisha ofisi zetu za mkoa,  kuimarisha mifumo ya tehema ikiwa ni pamoja na kuimaruaha usimamizi wa mashauri" alisema Mulwambo.

Ofisi ya waziri mkuu wa serikali kupitia wizara ya katiba na sheria  imeongezewa bajeti  kutoka  Bilion 12, 812, 816, 000 kwa mqaka wa fedha 2022/2023  hafi kufikia bilion 17, 075, 830, 000 kwa mwaka wa fedha 2023/2024  ikiwa ni ongezeko la asilimia 25.
Ofisi ya wakili mkuu wa serikali yaokoa mabilioni ya fedha. Ofisi ya wakili mkuu wa serikali yaokoa mabilioni ya fedha. Reviewed by Fahadi Msuya on October 13, 2023 Rating: 5