Header AD

header ads

REGROW YAAJIRI 178 MTEMERA



Na Sixmund Begashe

Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na kukuza Utalii Nyanda za juu Kusini mwa Tanzania (REGROW) umetoa ajira 178 kwa Watanzania kutoka  maeneo mbalimbali katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere kunakotekelezwa mradi huo.

Akizungumza na wanahabari ndani ya Hifadhi ya Nyerere juu ya matokeo chanya ya Mradi wa REGROW, Mwandisi Mshauri Mhando Jambia amebainisha kuwa kati ya ajira hizo, 78 ni za kudumu mpaka mwisho wa mradi huo ambao umeanza Mei 10, 2023 hadi Agosti 13, 2024 na ajira 100 ni za muda mfupi mfupi kulingana na mahitaji ya watu katika sehemu ya kazi za mradi huu. 

Mradi huo unahusisha ujenzi wa  majengo ya wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, kempu za watalii, geti la kuingia na kutokea mbugani Mtemere na nyumba za kulala watalii, ambapo ajira hizo ni tofauti na wale walioajiriwa kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Mtemere kilichopo Hifadhini humo.

Naye Muuguzi Bi Vaileth Mdotta,  anaefanya kazi kwenye utekelezaji wa mradi huo, ameishukuru Serikali chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa mradi wa REGROW kwa kuwa unewapatia ajira watanzania wengi hali inayo wawezesha kujimudu kimaisha pamoja na familia zao.
REGROW YAAJIRI 178 MTEMERA REGROW YAAJIRI 178 MTEMERA Reviewed by Fahadi Msuya on October 30, 2023 Rating: 5