Header AD

header ads

Tanzania yashiriki mkutano wa 74 wa UNHCR

NAIBU Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Jumanne Sagini  (kushoto) akiambatana na Sudi Mwakibasi (aliyekaa nyuma), Kaimu Naibu Mwakilishi wa kudumu Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu (kulia) wakifuatilia na kusikiliza hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa 74 wa Kamati Tendaji ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) ambao umeanza leo Oktoba 09 na utamalizika Oktoba 13, 2023 Geneva, Uswisi.

Na Mwandishi wetu

NAIBU Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Jumanne Sagini akiambatana na ujumbe wa Tanzania ameshiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa 74 wa kamati tendaji ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).

Katika Ufunguzi uliyofanyika leo Oktoba 09 Geneva, Uswisi Kamishina Mkuu wa UNHCR ameelezea changamoto ya kuongezeka kwa idadi kubwa ya Wakimbizi wakati huo fedha za kuwahudumia zikizidi kupungua na kutoa wito Kwa wafadhili kuwezesha kusaidia eneo hilo muhimu la usaidizi wa kibinadamu.

Mkutano huo umeanza leo tarahe 09 - 13 Oktoba 2023 Geneva, Uswisi ambapo Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Jumanne Sagini, amrongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo. 
Tanzania yashiriki mkutano wa 74 wa UNHCR Tanzania yashiriki mkutano wa 74 wa UNHCR Reviewed by Fahadi Msuya on October 09, 2023 Rating: 5