MAGU YAZINDUA RASMI WIKI YA MAGONJWA YASIOMBUKIZA , WANANCHI WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUPIMA AFYA BURE
Wananchiu wa Wilaya ya Magu wameshauriwa kuishi mtindo bora wa maisha unaozingatia ulaji unaofaa na kuepuka kula vyakula vyenye mafuta mengi , kuepuka matumizi ya pombe, uvutaji wa sigara , kuepuka msongo wa mawazo na kufanya mazoezi ya mwili ili kuepuka magonjwa yasioambukiza ambayo yameripotiwa kuchangia asilimia 74 ya vifo duniani kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya duniani ( WHO) mwaka 2022.
Wito huo umetolewa na mratibu wa magonjwa yasioambukiza Wilaya ya Magu Dokta Paulina Silvanus wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasioambukiza iliyofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Magu Jumatatu Novemba 6, 2023.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasioambukiza Dr Paulina amesema katika vifo vyote vinavyotokea Hospitali ya Wilaya ya Magu asilimia 30 husababishwa na magonjwa yasioambukiza hivyo amesisitiza kuwa wataendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuweza kuboresha na kurekebisha mfumo na mtindo wa maisha ili kupunguza magonjwa yasioambukiza.
Amesema kuwa Hospitali ya Wilaya imeweza kuanzisha kliniki ya magonjwa yasioambukiza kama vile presha , sukari na selimundu ambayo hufanyika kila siku ya jumatano na wastani wa wagonjwa 10- 15 huudhuria kliniki hiyo.
" Pia tumeweza kufanya huduma za mikoba za utoaji elimu na upimaji wa magonjwa yasioambukiza katika kata mbalimbali ndani ya Wilaya ya Magu" amesema Dr Paulina
Kuhusu changamoto Dr. Paulina amesema kuwa uwezo duni wa kumudu ghrama za matibabu hivyo kupelekea watu wachache kuhudhuria kliniki ya magonjwa yasioambukiza.
Kwa upande wake Kiongozi wa damu salama Wilaya ya Magu Lusekelo Charles amehimiza wananchi kujitoa kwa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu wengine sambamba na kujiwekea akiba pindi unapotokea uhitaji kwao binafsi.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali akiwemo Bi. Anna Jeremiah Mkazi wa Iseni na Bwa. Onesmo Makunu Mkazi wa Isandula wamepongeza utaratibu wa zoezi la upimaji wa afya bure linalofanywa na Hospitali ya Wilaya katika wiki ya magonjwa yasiombukiza na kuahidi kwenda kuhamasisha wananchi wengine kujitokeza kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali na kupatiwa ushauri wa kitaalamu.
Wilaya ya Magu imeanza kuadhimisha wiki ya magonjwa yasioambikiza ambapo leo Jumatatu Novemba 6, 2023 imeendesha shughuli mbalimbali ikiwemo zoezi la upimaji wa afya bure kwa wananchi, kutoa elimu ya magonjwa yasiyoambukiza , elimu ya lishe, macho, damu salama na elimu ya saratani mbalimbali zoezi hili ni la wiki nzima na linatarajiwa kukamilika siku ya jumapili Novemba 12, 2023
MAGU YAZINDUA RASMI WIKI YA MAGONJWA YASIOMBUKIZA , WANANCHI WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUPIMA AFYA BURE
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 07, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 07, 2023
Rating:




Post a Comment