Header AD

header ads

MIFUMO YA KIDIJITALI YA NHIF KUONGEZA UFANISI WA HUDUMA

Serikali imezindua mfumo wa kidijitali unaotarajiwa kuimarisha utoaji wa huduma za Bima ya Afya kupitia vifurushi vipya, ikiwemo Toto Afya Kadi. Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha watoto, ambao ni kundi muhimu, wanapata huduma bora.


Mifumo hii ya kidijitali, iliyotengenezwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 4.45, imeokoa Shilingi Bilioni 3.5 kwa kutumia wataalam wa ndani. Mfumo huo sasa unaweza kushughulikia folio 1,200 kwa dakika 45, ikilinganishwa na folio 800 kwa siku hapo awali.


Waziri Mhagama amesisitiza umuhimu wa ubora wa huduma, akielezea kuwa uzinduzi wa Toto Afya Kadi na vifurushi vingine kama Serengeti na Ngorongoro ni hatua kubwa kuelekea kufanikisha malengo ya afya kwa wote ifikapo 2030.


Aidha, ameelezea uwekezaji wa Serikali katika vifaa tiba na dawa ambapo upatikanaji wa dawa umefikia asilimia 86. Takriban vituo 9,826 vinatoa huduma za afya nchini, asilimia 75 kati ya hivyo vikiwa ni vya Serikali.

MIFUMO YA KIDIJITALI YA NHIF KUONGEZA UFANISI WA HUDUMA MIFUMO YA KIDIJITALI YA NHIF KUONGEZA UFANISI WA HUDUMA Reviewed by Fahadi Msuya on December 21, 2024 Rating: 5