NMB yakabidhi vifaa vya michezo kwa BAMMATA kuelekea michezo ya majeshi Zanzibar
Benki ya NMB imekabidhi msaada wa vifaa vya michezo kwa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya majeshi inayotarajiwa kuanza Septemba 6 jijini Zanzibar.
Msaada huo umekabidhiwa na Meneja Biashara wa Benki ya NMB Zanzibar, Naima Said Shaame, kwa Mwenyekiti wa BAMMATA, Brigedia Jenerali Saidi Hamis Saidi, katika hafla fupi iliyofanyika Zanzibar. Wengine walioshuhudia makabidhiano hayo ni Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite, Kanali Robert Mbuba na Luteni Kanali Said Shamhuna.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, uongozi wa NMB ulieleza kuwa msaada huo ni sehemu ya mchango wa benki katika kuunga mkono sekta ya michezo na afya, pamoja na kuimarisha mshikamano miongoni mwa askari kupitia michezo hiyo.
NMB yakabidhi vifaa vya michezo kwa BAMMATA kuelekea michezo ya majeshi Zanzibar
Reviewed by Fahadi Msuya
on
July 30, 2025
Rating:
Post a Comment