NMB yadhamini, yashiriki kikao cha wenyeviti wa bodi za taasisi za umma
Benki ya NMB imedhamini na kushiriki kwenye Kikao kazi cha wenyeviti wa Bodi na watendaji wakuu wa taasisi za umma (CEOs Forum
2025) kinachoendelea katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano Arusha (Arusha International Conference Centre).
Ujumbe wa NMB umeongozwa na David Nchimbi - Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi pamoja na Juma Kimori - Afisa Mkuu wa Fedha na Kaimu Afisa Mtendaji mkuu.
Kikao kazi hicho cha Siku tatu kinawashirikisha Viongozi zaidi ya Mia Sita Hamsini kutoka Taasisi, Mashirika na Wakala wa Serikali. Kauli mbiu ya Kikao hicho ni “Kujenga Ushirikiano Endelevu katika Mazingira ya Ushindani wa Kimataifa – Wajibu wa Mashirika ya Umma
NMB yadhamini, yashiriki kikao cha wenyeviti wa bodi za taasisi za umma
Reviewed by Fahadi Msuya
on
August 25, 2025
Rating:
Post a Comment