NMB JASIRI Yazinduliwa Rasmi Tanzania: Fursa Mpya kwa Wanawake na Wajasiriamali
Mpango wa NMB JASIRI wazinduliwa ukilenga kuwapa wanawake elimu ya fedha, ujasiri wa biashara na fursa za ukuaji. Sikiliza ujumbe wa Ruth Zaipuna
NMB JASIRI Yazinduliwa Rasmi Tanzania
Kuna ndoto nyingi za wanawake Tanzania, na sasa NMB JASIRI imezinduliwa rasmi kuzifungua.
Katika uzinduzi huu, Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, anawakaribisha wanawake kwenye Kochi la Jasiri – Kochi la Orange.
Ni nafasi ya kuzungumza, kushirikishana elimu ya fedha, na kufungua fursa mpya za kukuza biashara kwa wanawake nchini Tanzania.
Mpango wa NMB JASIRI unalenga kuwapa wanawake maarifa ya kifedha, kuimarisha ujasiriamali, na kuchochea maendeleo ya biashara zao.
Karibu JASIRI. Karibu Tuyajenge.
Tags: NMB Jasiri, Wanawake Tanzania, Ruth Zaipuna, Biashara Wanawake, Elimu ya Fedha