Header AD

header ads

COSTECH KUFANYA ' MEDIA DAY' KUIFAHAMISHA JAMII KAZI ZINAZOFANYWA NA TUME

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Dkt Amos Nungu akizungumza katika mkutano wa Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari juu ya Mwelekeo wa Wizara, Vipaumbele na Maeneo ya Kimkakati katika Utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2022/23  tarehe 29 Julai 2022 Jijini Dar es Salaam


Na Yusuph Digossi- Sauti za Mtaa Blog

Dar es Salaam

Katika kutambua mchango mkubwa  wa Waandishi wa habari kwenye jamii iwe ni kuhabarisha au kuelimisha haswa katika maendeleo ya Sayansi na Teknlojia, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknlojia COSTECH imekusudia kuja na siku maalumu ya Waandishi wa habari 'MEDIA DAY' kwa lengo la kuifahamisha jamii kazi zinazofanywa na COSTECH.

Hayo yamebainishwa na  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Dkt Amos Nungu  katika mkutano wa Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari juu ya Mwelekeo wa Wizara, Vipaumbele na Maeneo ya Kimkakati katika Utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2022/23  tarehe 29 Julai 2022 katika ofisi za COSTECH Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Nungu amesema kuwa Tume imekuwa ikijifunza  kila siku namna ya kufanya kazi na wanahabari ikiwemo kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wanahabari kwa lengo la kuwafahamisha namna bora ya kufikisha taarifa za COSETCH katika jamii haswa kueleza miradi iliyopo katika kanda husika.

"Mwaka jana tulifanya Kanda ya Kaskazini , Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha na mwaka huu tuliita wahahari wa vyombo vya habari ili kuendelea kuona namna gani tunafanya kazinpamoja na kazi tunazozifanya zifike kwa wananchi wengi zaidi na njia zilizosahihi" amesema Dkt. Nungu" 

Ameongeza kuwa Serikali inafanya mambo mengi kupitia COSTECH lakini hayajulikani sana hivyo kupitia vyombo vya habari wananchi watapata taarifa na kujua zaidi kazi zinazofanywa na tume ya Sayansi nchini Tanzania.

Amesema kuwa siku hiyo wamekusudia kuifanya tarehe 16-08-2022 ambapo kutakuwa na bidhaa mbalimbali za utafiti na ubunifu ambazo zitaoneshwa kwa wanahabari ili kuhabarisha umma kufahamu kazi zinazofanywa na COSTECH.
COSTECH KUFANYA ' MEDIA DAY' KUIFAHAMISHA JAMII KAZI ZINAZOFANYWA NA TUME COSTECH KUFANYA ' MEDIA DAY'  KUIFAHAMISHA JAMII KAZI ZINAZOFANYWA NA TUME Reviewed by Fahadi Msuya on July 30, 2022 Rating: 5