Nape aongeze kasi mchakato mabadiliko ya sheria ya habari
Na Yusuph Digossi
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amemkumbusha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kuongeza kasi katika mchakato wa mabadiliko wa sheria ya habari nchini lengo kuondoa baadhi vipengele vya sheria hiyo ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wadau wa habari nchni kwa kuminya uhuru wa vyombo vya habari.
Pia Balile amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu kwa kuona umuhimu wa kupitia sheria za habari na kuagiza zifanyiwe maboreshio ili kuendana na mazingira yaliyopo.
Balile ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Clouds TV tarehe 28 Julai 2022 Jijini Dar es Salaam.
Balile amebainisha kuwa endapo mchakato huo wa mabadiliko ya sheria ukikamilika utaleta uhuru wa habari hapa nchni bila kuumiza mwengine.
" Mchakato huu huu haulengi upendeleo kwa wanahabari bali haki, wajibu na mazingira mazuri wa Tasnia ya habari hapa nchni " amesema Balile.
“Tufahamu kuwa uhuru wa habari ni haki ya msingi ambayo wengi wanaitaka. Vyombo vya habari visipokuwa huru, wananchi nao pia wanakosa uhuru ikiwa ni pamoja na kutoa maoni yao pia kupata taarifa zinazowahusu moja kwa moja,” amesema.
“Tunapozungumzia uhuru wa vyombo vya habari, sio kwamba tunataka upendeleo kutoka serikalini, la! Tunacholenga hapo kila mmoja apate haki na awajibike,” ameongeza Balile.
Nape aongeze kasi mchakato mabadiliko ya sheria ya habari
Reviewed by Fahadi Msuya
on
July 30, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
July 30, 2022
Rating:

Post a Comment