MAANDALIZI YA TAMASHA LA REJOICE YAZIDI KUPAMBA MOTO, WAZIRI NAPE MGENI RASMI
Dar es Salaam
Maandalizi ya tamasha la Kusifu na Kuabudu la Rejoice chini ya kwaya Moravian Efatha Choir yanayoendelea katika uwanja wa Uhuru ambapo yanatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaaa Septemba 16 Mwaka huu yamepambamo na kufikia Asilimia 95
Tamasha hilo la aina yake na la kipekee kuwahi kufanyika hapa Tanzania linatarajiwa kuwakutanisha wasanii mbalimbali wa nyimbo za injili huku macho na masikio ya watu wengi yakiwa kwa kwaya ya Joyous celebration kutoka Afrika Kusini.
Akieleza yalipofikia maandalizi ya Tamasha hilo mbele ya Waandishi wa Habari Leo Tarehe 13 Katika Uwanja wa Uhuru mlezi wa kwaya ya Moravian efatha Yona Sonelo amesema maandalizi yamefikia Asilimia 95 Katika kuelekea siku ya tamasha.
"Siku ya Tamasha tarehe 16 ya mwezi wa tisa Mgeni Rasmi atakuwa ni waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Moses Nnauye"Amesema Yona.
Ameongeza kuwa tiketi Bado zinapatikana Katika app ya NILIPE ambapo zinaanzi Shilingi Elfu ishirini, Elfu Ishirini, Elfu Hamsini , VIP Laki Moja, VIP Laki tano na VVIP millioni moja.
Kwa upande wake muandaaji wa muziki wa Injili kutoka Neem Gospel Kwaya Fredrick Masanja emesema kuwa kundi lao limejiandaa vizuri kutoa burudani kwa watakaohudhuria tamasha hilo huku akitoa wito kwa Watanzania kuendelea kununua tiketi na kuhudhuria Tamasha hilo kwaajili ya kutukuza neno la Mungu.
Naye Bupe Jimmy Mwakusya ambaye ni Mwanakwaya wa ambaye ni mwana Survivor Kwaya amesema amewaalika Watanzania wote kuhudhuria Tamasha hilo ili kuendeleza Amani ya Watanzania na kutukuza neno la Mungu.
MAANDALIZI YA TAMASHA LA REJOICE YAZIDI KUPAMBA MOTO, WAZIRI NAPE MGENI RASMI
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 13, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 13, 2022
Rating:





Post a Comment