MEENA: HATUA ZILIZOCHULIWA NA RAIS SAMIA ZIMEONGEZA ARI KWA WADAU WA HABARI
SHERIA ya habari ya mwaka 2016 ilianza kulalamikiwa kwa kipindi kirefu na wadau wa habari kwa kuwa haikuondoa mitego iliyowekwa na sheria ya mwaka 1979 na kuchangia kudumaa kwa vyombo vya habari nchini.
Hayo yamesemwa leo na Neville Meena ambaye ni mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), wakati akizungumza katika Kipindi cha Front Page kinachorushwa na Radio +255 Global jijini Dar es Salaam.
Meena amesema kuwa sheria hiyo ilianza kupigiwa kelele kwa muda mrefu na wadau wa habari ambapo Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan iliona haja ya kukaa meza moja na wadau wa habari ili kuipatia ufumbuzi.
Amesema, hatua za awali alizochukua Rais Samia Suluhu Hassan,ziliongeza ari ya wadau wa habari kushirikiana ili kung’oa vipengele hasi vya sheria ya habari.
‘‘Hatua zilianza kuchukuliwa kwa serikali kuleta mapendekezo ya maeneo ya kurekebisha, lakini na sisi tuliongeza yetu ambayo wao walikuwa hawajaweka kwenye mapendekezo yao kwa kuwa mabadiliko hayo yalianzia kipengele cha 38.
“Sheria ya Habari ya Mwaka 1976, imefanya kazi kwa miaka 40, muda wote huo imetoa mwanya kwa mtu mmoja (waziri) kufungia chombo cha habari anapojisikia kufanya hivyo
Hata Sheria ya Habari ya Mwaka 2016 ilipotungwa, imefuata mkondo huo huo wa kutoa mamlaka kwa mtu mmoja kuamua kufungia chombo cha habari ama la ingawa mamlaka hayo amepewa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Malelezo.Katika mabadiliko haya, tumeiomba serikali iondoe kipengele hicho,’’amesema Meena.
MEENA: HATUA ZILIZOCHULIWA NA RAIS SAMIA ZIMEONGEZA ARI KWA WADAU WA HABARI
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 15, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 15, 2022
Rating:

Post a Comment