WAKULIMA WA MKONGE WAKABILIWA NA UHABA WA MASHINE ZA KUCHAKATA MKONGE.
Na Robert Benjamini
Mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba ameishauri benki ya NMB pamoja na taasisi zote za kifedha zilizopo kuendelea kutoa mikopo kwa wafanyabiashara na wakulima hii ikiwa ni pamoja na kuwawezesha vifaa vya umwagiliaji vitakavyowasaidia kuondokana na kilimo cha kutegemea msimu wa mvua.
Mgumba ametoa wito huo kwa taasisi za kifedha wakati akizindua tawi jipya la benki ya ya NMB Ngamiani lililopo jijini Tanga ambapo alisema kuwa yapo maeneo mengi yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji hekta zaidi ya Millioni 2 huku changamoto kubwa kwa wakulima ikiwa ni ukosefu wa vifaa vinavyoweza kujikita katika sekta hiyo itakayowasaidia kujipatia maendeleo na hatimaye kuweza kuchangia pato la Taifa.
"Tunazo zaidi ya hekta millioni mbili zinazofaa kwa umwagiliaji na maji yapo lakini mpaka sasa ni kati ya hizo tumeweza kuendeleza na kuwekeza kwenye hekta laki sita na sitini tu ombi langu kwa taasisi zote za fedha na mabenki yote angalieni Sera zenu kuanza kukopesha kwenye sekta ya umwagiliaji ili tutatue changamoto kwa wakulima ya kutegemea kilimo cha mvua ili hatimaye wawe na uhakikia na kipato na uwekezaji wao kwenye sekta ya kilimo" alisema Mgumba.
Aidha kufwatia upanuzi wa Bandari ya Tanga wa kuongeza kina cha bahari ambao unatarajiwa utakapokamilika mwezi November utakuwa na uwezo wa kumhudumia shehena ya mizigo ipatayo tani millioni tatu kwa mwaka amezitaka taasisi hizo kuwakopesha wafanyabiashara na wawekezaji watakaoweza kujenga maghala ya kuhifadhia shehena hiyo hatua ambayo itasaidia kuitangaza Bandari hiyo kimataifa.
"Katika Bandari yetu ya Tanga tumeongeza kina kutoka mita 3 mpaka 13 na sasa hivi tunaweza kushusha Meli nne kwa pamoja na mradi utakapokamilika tutaweza kushusha shehena million tatu kwa mwaka kutoka Taki laki saba kwa Sasa ,uwekezaji huo mkubwa uliofanywa na serikali katika Bandari yetu umeleta fursa nyingine katika sekta ya uhifadhi wa mizigo lakini hatuna maghala ya kuhifadhia shehena hiyo wito kwa NMB ni kutoa mikopo kwa wafanyabiashara na wawekezaji ili waje kuwekeza ujenzi wa maghala" aliongeza
Awali akizungumza meneja wa uchumi na takwimu kutoka benki kuu ya Tanzania kanda ya Kaskazini Ernest Ndunguru amebainisha kuwa kumekuwa na changamoto kwa taasisi za kifedha kushindwa kuwahudumia wateja wake hasa kipindi cha sikukuu na wikiendi huku akiipongeza benk hiyo kwa kuendelea kupeleka huduma zake karibu na jamii akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi zote za kifedha hapa nchini.
"NMB kufungua tawi jipya ni ishara ya kuonyesha kwamba wapo bega kwa bega na BOT katika kutekeleza sera za fedha na kuhakikisha mzunguko wa fedha na huduma zingine zinawafikia wananchi , kumekuwa na utamaduni wa mabenki kushindwa kuwahudumia wateja wake hasa siku za sikukuu na wikiendi hili ni tatizo la karibuni benki nyingi ni vizuri changamoto hii ikatiliwa maanani" alisema Ndunguru
"Sisi Benki kuu ya Tanzania ambao ni wasimamizi wakuu wa benki na taasisi zote za kifedha tutaendelea kuwaunga mkono mabenki yote ili kuhakikisha ustawi wao unaimarika na hautetereki" aliongeza.
Kwa upande wake afisa mkuu wa NMB anayesimamia wateja wakubwa wa serikali na taasisi zake Alfred Shayo alisema kuwa wameendelea kuwawezesha kuwainua watanzania kupitia sekta ya kilimo ambapo wameweza kutoa shilingi bilioni 100 pamoja na kuirejesha asilimia 1 kwa jamii huku wakitoa gawio la shilingi bilioni 30.9 kwa serikali mwaka jana.
"Benki ya NMB tumefanya kazi kwa karibu sana na serikali pamoja na wateja wetu kwa upande wa Kanda ya Kaskazini tuna matawi 40 kwenye upande wa kilimo tulitenga shilingi bilioni 100 ambazo tulikopeasha kwa wakulima wadogowadogo kwa riba isiyozidi 9%, tumekuwa na deaturi pale tunapopata faida tunarudisha 1% kwa jamii na kwa mwaka jana tultoa gawio kwa serikali kiasi cha bilion 30.9 mwak"
Sambamba na hayo benki ya NMB iliweza kutoa mabati 250 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa shule ya msingi Masiwani iliyopo jijini Tanga kama sehemu ya kurudusha faida waliyoipata kwa jamii.
WAKULIMA WA MKONGE WAKABILIWA NA UHABA WA MASHINE ZA KUCHAKATA MKONGE.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 15, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 15, 2022
Rating:








Post a Comment