RASIMU YA MTAALA YAWASILISHWA KWA WADAU
Kamati ya Kitaifa ya Uboreshaji Mitaala leo tarehe 27/09/2022 imewasilisha rasimu pendekezwa ya mitaala ya Elimu ya Awali, ElimuMsingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu kwa wadau mbalimbali wa Elimu.
Kikao hicho kimefanyika Jijini Dodoma katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi na kuhudhuriwa na Wabunge, Timu ya Zanzibar inayoshughulikia Sera na Mitaala, Vyuo Vikuu, Taasisi za Dini, BAKITA, Wadau wa Maendeleo na Wathibiti ubora wa shule.
Mapendekezo ya Rasimu yamewasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati Prof. Makenya Maboko na Kamati imepokea maoni mbalimbali kutoka wa wadau na kuahidi kuyafanyia kazi katika maboresho ya Mitaala yanayoendelea.
RASIMU YA MTAALA YAWASILISHWA KWA WADAU
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 27, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 27, 2022
Rating:




Post a Comment