WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YASHEREKEA SIKU YA UTALII DUNIANI KWA TUZO ZA TANAPA
Katika kuadhimisha Siku ya Utalii Duniani, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, baada ya kukabidhi Mitambo na Magari yatakayotumika kukarabari miundombinu ya Hifathini, usikuu wa tarehe 27 Septemba 2022 amekabidhi Tuzo za Tatu za Utalii za Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa wadau mbalimbali wa utalii katika hafla iliyofanyika jijini Arusha.
Katika Tuzo hizo, Mwenyekiti wa Bodi ya TANAPA, Jenerali Mstaafu, George Waitara, amekabidhi Tuzo maalum kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, liyopokelewa kwa niaba yake na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, inayotambua mchango Mkubwa wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Utalii nchini hasa kupitia Filamu ya The Royal Tour.
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YASHEREKEA SIKU YA UTALII DUNIANI KWA TUZO ZA TANAPA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 28, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 28, 2022
Rating:





Post a Comment