Header AD

header ads

SAMAF wakabidhi msaada wa taulo za kike za kufua 50 kwa wanafunzi walemavu Kigamboni

 



Na Mwandishi wetu 


UMOJA wa Wanahabari Wanawake chini ya Asasi ya Sauti ya Matumaini (SAMAF) umetoa msaada wa taulo za kike za kufua  50 kwa wanafunzi 50 walemavu waliopo katika Shule ya Msingi Maalum ya  Kigamboni, Maweni na Vijibwemi zote za jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuungana na Serikali kulisaidia kundi hilo.



Msaada huo wa taulo za kike  umekabidhiwa jana shuleni hapo ambao umeenda sambamba na utoaji wa elimu ya hedhi salama na namna bora ya kuzitumia taulo hizo za kufua.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa SAMAF, Mary Geofrey alisema kupitia msaada huo kila mwanafunzi wa kike katika shule hizo tatu atapata taulo hizo ambazo atazitumia kwq zaidi ya miaka miwili.


Geofrey alisema wanaamini kupitia taulo hizo za kike zitawafanya wanafunzi kuwa nadhifu, kuwaongezea tabasamu, kujiamini na hari ya kupenda masomo itakayochochea na kuongezeka kwa ufauli katika madarasa yao.




"Mradi wetu huu tulianza na shule mbili wilayani Temeke, ambazo ni Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu na Mtoni Maalum na jumla ya wanafunzi 100, tuliwafikia na kuwapatia taulo za kike 1,000 pamoja na elimu ya kujitambua na kujithamini.



"Leo (jana) tumezikia shule tatu za Kigamboni na watoto hawa wamepata bahati ya kupatia ralo za kufua ambazo watadumu nazo kwq zaidi ya miaka miwili na kuwapunguzia mzigo kwa wazazi na walezi wao wa kununua zile za dukani kila mwezi,"  alisema Geofrey 


Aidha alisisitiza kuwa SAMAF ni umoja wa Wanahabari Wanawake, walioamua kujitoa kurudisha tabasamu kwa jamii kwa njia ya vitendo, badala ya kutumia kalamu peke yake huku wakiwa na  Kauli mbiu ya ‘Nilinde ithamini Kesho Yangu’.


Naye Katibu wa SAMAF, Janeth Jovin alisema watoto wa kike wanaotokea kwenye familia duni mara nyingi hukosa kuhudhuria masomo wanapokuwa katika siku za hedhi kutokona na kukosa vifaa salama vya kujihifadhia kama taulo au pedi kama wengi wanavyoita.


Alisema msaada wa taulo hizo utakwenda kuwarudishia tumaini watoto hao wa kike na kuondoa changamoto hiyo ambayo inawakabili pindi wanapoingia katika siku zao za hedhi. 

"Mradi wetu unafanyika chini ya kampeni yake yenye kauli mbiu ya 'Ithamini na Ilinde kesho tunaratajia kuwafikia watoto wengi zaidi wenye ulemavu waliopo kwenye maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Dar es Salaam," alisema


Awali mgeni rasmi katika tukio la ugawaji wa taulo hizo,  Ofisa Elimu, Elimu Maalum Halmashauri  ya Manispaa ya Kigamboni,Joshua Samson alisema wanaipongeza asasi ya SAMAF kwa kutoa msaada huo kwa wanafunzi hao na anaamini jambo hilo litakuwa endelevu. 


"Tunaamini tukio hili lililofanyika litakuwa endelevu na niwaombe wamama wenye watoto walemavu wasiwafiche majumbani, wawalete katika shule maalum zilizopo katika kila manispaa ili wachanganyike na wenzao ili kupata maarifa mapya," alisema 



Naye Mwalimu wa Elimu Maalum wa Shule ya Msingi Maweni,Fatuma  Selemani aliishukuru SAMAF kupitia taasisi ya Tabasamu ya nchini Ujerumani kuwasaidia watoto wenye ulemavu taulo hizo ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwao pindi wanapoingia katika Hedhi. 


"Tunawashukuru sana kwa kujitoa kwenu tunaomba wadau wengine wajitokeze kusaidia makundi haya kwani yanachangamoto nyingi ambazo Serikali pekee haiwezi kuzimaliza,"alisema 


SAMAF wakabidhi msaada wa taulo za kike za kufua 50 kwa wanafunzi walemavu Kigamboni SAMAF wakabidhi msaada wa taulo za kike za kufua 50 kwa wanafunzi walemavu Kigamboni Reviewed by Fahadi Msuya on September 26, 2022 Rating: 5