WABUNIFU WA TEHAMA KUNIFAIKA NA KONGAMANO LA KIBIASHARA BAINA YA TANZANIA NA DRC
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu Kongamano la Fursa za Kibiashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo tarehe 26 Septemba, 2022 jijini Dar es Salaam.
Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Nchini Tanzania, Bw. Kanupangi Yamba Gilbert akuzungumza wakati wa mkutano na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu Kongamano la Fursa za Kibiashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo tarehe 26 Septemba, 2022 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akizungumza na Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Nchini Tanzania, Bw. Kanupangi Yamba Yamba Gilbert muda mchache kabla ya kuzungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu Kongamano la Fursa za Kibiashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo tarehe 26 Septemba, 2022 jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu Dar es Salaam
Serikali kupitia wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imewahakikishia wabunifu wa TEHAMA fursa ya kutangaza bidhaa zao kupitia kongamano la fursa la mashirikiano baina ya Tanzania na Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC) kwenye sekta ya mawasiliano.
Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika DRC.
Amesema kupitia kongamano hilo la fursa ya mashirikiano kwenye sekta ya mawasiliano, mambo mabalimbali yatajadiliwa ukiwemo mpango wa kuiunganisha DRC na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kurahisisha huduma za mawasiliano kwa wafanyabishara na wabunifu wa TEHAMA.
Aidha Waziri Nape amebainisha kuwa kongamano hilo litazisaidia kampuni changa kupata fursa ya kutambulika kimataifa, hivyo amewasisitiza wabunifu kushiriki kwa wingi.
Kwa upande wake kaimu Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo nchini Kanupangi Yamba Yamba Gilbert, ameahidi ushirikiano katika kufanikisha kongamano hilo muhimu kwa ustawi wa pande hizo mbili.
Takribani kampuni hamsini za ubunifu za huduma ya TEHAMA zinatarajiwa kushiriki katika kongamano hilo litakalofanyika Oktoba 18 na 19 mwaka huu huko Lubumbashi.
WABUNIFU WA TEHAMA KUNIFAIKA NA KONGAMANO LA KIBIASHARA BAINA YA TANZANIA NA DRC
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 26, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 26, 2022
Rating:




Post a Comment