UVCCM ANANASIF YAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA KUHAMASISHA MICHEZO
Mwenyekiti wa UVCCM kata ya Ananasif Kinondoni Jijini Dar es Salaam Bwa. Ibrahi Stephano John akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa Bonanza la mpira wa miguu leo Jumamosi Septemba 03 2022.
Mwenyekiti wa UVCCM kata ya Ananasif Kinondoni Jijini Dar es Salaam Bwa. Ibrahi Stephano John akiwa katika mazoezi ya Kukimbia (Jogging) mapema leo Asubuhi kabla ya kuanza kwa Bonanza la Mpira wa Miguu lililofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ananasif
Na Yusuph Digossi
Na Yusuph Digossi
Vijana wametakiwa kujijengea tabia ya kushiriki michezo mbalimbali kila mara badala ya kujiingiza katika makundi mabaya ya wizi pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevya kitu ambacho kinawaaribia mfumo mzima wa maisha yao.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa UVCCM kata ya Ananasif Kinondoni Jijini Dar es Salaam Bwa. Ibrahi Stephano John wakati wa Bonanza la Michezo wa mpira wa miguu ambalo liliambatana na mazoezi ya kukimbia "Jogging" ambalo limefanyika leo Jumamosi Septemba 03 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ananasif Jijini Dar es salaam.
Bonanza hilo limeandaliwa na umoja wa Vijana Kata ya Ananasif kwa kushirikiana na viongozi wengine wakimemo wajumbe wa Baraza na Kamati ya Utekelezaji , Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti huyo amesema kuwa lengo la kuandaa Bonanza hilo ni kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu kuhamasisha michezo.
Katika Bonanza hilo jumla ya timu 4 kutoka katika kata 4 za Manispaa ya Kinondoni zimeshiriki ikiwemo Kata ya Ananasif, Mwananyamala, Makumbusho na Kinondoni amabapo mshindi wa Kwanza ataondoka na zawadi ya seti moja ya jezi na mshindi wa pili atapata mpira mmoja.
Amesema lengo lingine la kuandaa Bonanza hilo ni kuendeleza Umoja, mshikamano na ujirani mwema kati ya viongozi na Wananchama wa Chama Cha Mapinduzi ambao ni Vijana.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kinondoni Farida Iguni ameshauri michezo kama hiyo iwe endelevu ili kuendelea kuwaunganisha Vijana wa Manispaa ya Kinondoni huku akibainisha kuwa Michezo ni furaha na hulinda Afya za watu.
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kinondoni Farida Iguni akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa Bonanza la mpira wa miguu leo Jumamosi Septemba 03 2022.
Naye Mariam Martin Moto ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM kata ya Makumbusho amempongeza Mwenyekiti wa Ananasif kwa kuandaa bonanza hilo la ujirani Mwema ambalo litachagiza kuunganisha vijana wa Manisapaa ya Kinondoni ambayo ina kata 20.
UVCCM ANANASIF YAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA KUHAMASISHA MICHEZO
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 03, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 03, 2022
Rating:




Post a Comment