Header AD

header ads

Waziri Mchengerwa atakia Kila la heri Mwakinyo.




Na John Mapepele


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Mhe. Mohamed Mchengerwa anamtakia kila la heri bondia namba mmoja nchini  wa ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo anayetarajia kupanda ulingoni majira ya saa tatu usiku wa leo dhidi ya Muingereza, Liam Smith katika pambano la raundi 12, uzani wa Super Walter.

Akiongea mchana wa leo Septemba 3, 2022 amesema kuwa watanzania wana imani kubwa na bondia huyo kwamba anakwenda kuwa balozi wa Tanzania Kimataifa.

Ametaka kutanguliza uzalendo wa nchi yake ili kuendelea kushinda na kutangaza Tanzania duniani.

Amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuendeleza wanamichezo na timu za taifa  zinazofanya vizuri  ili zifanye vizuri zaidi.

Aidha amefafanua kuwa michezo ni uchumi na kwamba endapo itafanyika  vizuri itakwenda kuchangia kwenye uchumi wa nchi yetu.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mchengerwa amewataka wachezaji wengine  waige mfano wa bondia huyo ili kupata ajira na kuinua yao na familia zao.

Pambano hilo limepangwa kuchezwa kwenye ukumbi wa M & S Bank Arena uliopo katika Jiji la Liverpool nchini Uingereza.
Waziri Mchengerwa atakia Kila la heri Mwakinyo. Waziri Mchengerwa atakia Kila la heri Mwakinyo. Reviewed by Fahadi Msuya on September 03, 2022 Rating: 5