WAZIRI MCHENGERWA- SERIKALI KUMWAGA VIWANJA VYA KIMATAIFA KILA KONA.
Na John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali kupitia Wizara anayoiongoza inakwenda kukarabati viwanja vyake katika kiwango cha kimataifa ili viweze kutumika kwenye mashindano ya kimataifa.
Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Bungeni wakati akitoa majibu ya nyongeza kwenye swali aliloliuliza na Mhe. Festo Sanga, Mbunge wa Makete aliyetaka kujua fedha iliyopitishwa na Serikali kwa ajili ya kuweka nyasi bandia kwenye viwanja vya michezo.
Amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuhakikisha kuwa miundombinu ya michezo inaboreshwa na inakuwa ya kisasa zaidi.
Viwanja ambavyo vilipangiwa kukarabatiwa ni pamoja na viwanja vya Benjamini Mkapa, na uhuru vya Jijini Dar es Salaam, Arusha, Tanga, Mwanza, Mbeya na Dodoma.
Mbali na kufanya ukarabati wa viwanja hivyo pia serikali inakwenda kutengeneza miundombinu ya michezo kwenye shule mbili katika kila mkoa ili kuibua vipaji vya michezo.
Aidha, tayari Mhe. Waziri kwenye mikutano kadhaa na wadau wa michezo ikiwa ni pamoja na Kikao cha wadau wa Baraza la Michezo na kikao cha viongozi wa vilabu vya michezo amehimiza kila timu kuwa na kiwanja cha michezo kulingana na matakwa ya sera ya michezo ambapo vilabu vyote vilikubali kuwasilisha mpango wa ujenzi WA viwanja hivyo katika kipindi cha miezi sita kuanzia mwezi Agosti mwaka huu.
WAZIRI MCHENGERWA- SERIKALI KUMWAGA VIWANJA VYA KIMATAIFA KILA KONA.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 13, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 13, 2022
Rating:


Post a Comment