WAZIRI MKENDA AZINDUA TUZO YA TAIFA YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amezindua rasmi Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu yenye lengo la kutambua mchango wa waandishi bunifu katika kukuza na kueneza lugha ya kiswahili Duniani uliofanyika jijini Dar es salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda
alisema; waandishi bunifu wamekuwa na mchango mkubwa katika kukuza nakueneza lugha ya kiswahili dunia na wamekuwa chachu katika kuelimisha
jamii inayo tuzunguka hivyo wanapaswa kupewa heshima na kuthaminiwa kwasababu waandishi bunifu ni jeshi linalo tumia kalamu.
''washindi watapata tuzo pamoja na fedha taslimu, kwa mshindi wa kwanza atapata kiasi cha shilingi millioni 10, mshindi wa pili atapewa kiasi cha shilingi millioni 7 na mshindi wa tatu ataibuka na kiasi cha
fedha shilingi millioni 5''. alisema mkenda.
Kwa upande wake mwenyekiti wa tuzo hizo Prof. Penina Mlema alitaja vigezo vya waaandishi bunifu kushiriki katika tuzo hizo ni pamoja na kuwasilisha nakala moja kwa kila kipengele ulicho chagua pia alisema nakala hiyo ni lazima iwe na hatimiliki ya mshiriki wa kipengele
hicho.
'' Washiriki wote wa tuzo hizi ni lazima wawasilishe nakala zao moja
kwa kila kipengele ulichochagua hairuhusiwi kuwasilisha nakala zaidi
ya moja pia ni lazima kila nakala ya Riwaya au ushairi iwe na hatimiliki ya mshiriki''. alisema Penina
Aidha Penina alisema; kuwa tuzo hizo zitakuwa ikitolewa kila mwaka
tarehe 13 April ikiwa ni siku ya kuzaliwa ya Mwalimu Nyerere pia amesma lengo la tuzo hiyo ni kuwatambua na kuwa zawadia waandishi bunifu, kukuza na kuinua vipaji na kukuza uchapishaji na uandishi bora tuzo zitolewa katika vipengele viwili tu navyo ni Riwaya na Mashairi.
''Tuzo zitakuwa zikitolewa kila mwaka tarehe 13 April ikiwa ni siku ya
kumbukizi ya kuzaliwa kwa Mwalimu Nyerere tuzo zikiwa na malengo ya
kuwatambua na kuwazawadia waandishi bunifu, kukuza na kuinua vipaji na
kukua uchapishaji na uandishi bora''. Aliongeza kuwa mwakani tuzo hizo
zitaongezwa vipengele vya hadithi za watoto pamoja na hadithi fupi
fupi''. Alisema Penina
Mwandishi mkongwe wa riwaya na kamusi Shafi Adam Shafi alimshukuru waziri mkenda pamoj na wizara yake kwa
kuanzaisha tuzo hizo kwani zitaongeza chachu ya waandishi kuona kama wanathaminiwa na kukumbukwa pia mchango wao katika nchi unaonekana pia
ameshauri tuzo hizo ziwe na muendelezo zisiishie hapo.
WAZIRI MKENDA AZINDUA TUZO YA TAIFA YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 12, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 12, 2022
Rating:





Post a Comment