HANDENI , KILINDI ZATAJWA KUONGOZA UTENGENEZAJI SILAHA ZA MOTO
Na Hadija Bagasha Tanga,
Wilaya ya Handeni na Kilindi zimetajwa kama wilaya zinazoongoza kwenye utengenezaji wa silaha za moto jambo ambalo limekuwa likihatarisha usalama wa watu sambamba na wanyama kwenye hifadhi za Taifa zinazopakana na maeneo hayo ikiwemo tembo.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Safia Jongo ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kusalimisha silaha haramu kwa hiari iliyofanyika Mkoani Tanga na kushirikisha wadau mbalimbali wa usalama.
"Handeni Kilindi wazigua wenzangu wana tabia ya kumiliki gobole kama mlinzi wanazitengeneza wenyewe hilo gobole umelitengeneza lakini unalimiki kinyume na visivyo halali wakati muafaka umefika isalimishe silaha yako kwa Mwenyekiti wa serikali za mtaa mwambie mimi nilichonga gobole kama mila lakini kwa sasa ninajua sio halali naiwasilisha silaha hii, "alisema Kamanda Jongo.
Kamanda Jongo amesema urejeshaji wa silaha hizo utamsaidia mmiliki mwenyewe pamoja na jamii kwasababu kumiliki silaha isivyo halali kunaweza kuchangia kufanyika kwa matendo ya uhalifu wa watu kwa kutumia silaha panoja na wanyama.
Kamanda Jongo alibainisha kuwa kumekuwa na matukio mbalimbali yanayohusishwa na matumizi ya silaha kinyume cha sheria ikiwemo mauaji ya wanyama na mengine ya kiuhalifu ambapo katika jitihada walizoendelea kuzichukuwa walifanikiwa kukamata silaha 62 na watuhumiwa 63 wakikamatwa kwa kipindi cha kuanzia January Hadi june 2022.
Jongo alisema kufwatilia uzagaaji wa silaha Tanga ni miongoni mwa mikoa mabayo unaweza kuathirika moja kwa moja katika mauaji na uwindaji haramu wa wanyama mbalimbali .
"Tanga itakuwa ni moja wapo ya mikoa ambayo itaathirika endapo kutakuwa na uzagaaji wa silaha kwani kutakuwa na vitendo vya uhalifu Kama mauaji na uwindaji haramu, mapori yetu mengi Yana wanyama silaha hizo zimekuwa zikitengenezwa kienyeji , kwahiyo urasimishaji wa silaha utatusaidia na utajisaidia mwenyewe na kjisaidia jamii kwa sababu kumiliki silaha visivyo halali utafanya matendo ambayo yatatuletea shida Kama uhalifu wa wanyama na matukio mengi ambayo yanatumia silaha" alisema Jongo.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha usimamizi na udhibiti wa silaha na leseni makao makuu ya jeshi la polisi Renada Milanzi amesema silaha zinazosalimishwa ni pamoja na zilizoingizwa nchini kinyume na sheria.
Milanzi amesema kuwa katika kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama hapa nchini hatua za maksudi zimechukuliwa kwa kushirikiana makundi mbalimbali katika kutekeleza kampeni hiyo baada ya serikali kutoa tangqzo la msamaha kwa yeyote atakayesalimisha silaha kwa hairi hatoshitakiwa.
"Jukumu la usalama ni la kila mwananchi hivyo Basi Polisi kwa kushirikiana na wadua wa ndani na nje kimeona umuhimu wa kuwashirikisha makundi mbalimbali katika jamii ili kutekeleza kampeni ya mwezi wa msamaha wa kurasimisha silaha kwa hairi ili kuimarisha usalama wa Taifa letu kampeni hii inaendelea nchi nzima na atakayesalimisha hatoshitakiwa
Awali akizindua kampeni hiyo kwa niaba ya Mkuu wa MKoa Tanga Omari Mgumba, Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Kanal Maulid Sulumbu amesema zoezi hilo linalenga kuimarisha hali ya usalama nchini.
Kanal Sulumbu amesema silaha haramu ndio chanzo kikubwa cha kuvunja amani na kurudisha maendeleo nyuma hivyo jamii inapaswa kushirikiana na jeshi la polisi kuzifichua silaha hizo.
Jeshi la polisi Nchini limetoa msamaha kwa wamikili wa silaha haramu Nchini Tanzania na kuwataka wale wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha kwa hiari yao kabla sheria haijachukua mkondo wake.
Mkoa wa Tanga ni moja kati ya mikoa mitatu iliyochaguliwa kama Mkoa darasa kwenye kampeni za Mwaka 2022 huku Mikoa mingine ikiwa ni Morogoro na Tabora.
Zoezi hilo ambalo ni kwa mara ya pili kufanyika hapa nchini kuanzia mwaka huu lilizinduliwa na Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Jumaanne Abdallah jijini Dodoma September 1 ambapo litendelea hadi October 31 , 2022.
HANDENI , KILINDI ZATAJWA KUONGOZA UTENGENEZAJI SILAHA ZA MOTO
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 12, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 12, 2022
Rating:








Post a Comment