WAZIRI MULAMULA APOKEA BARUA ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA KONSELI MKUU WA KENYA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb.), amekutana na kupokea barua za utambulisho kutoka kwa Konseli Mkuu wa Kenya mwenye makazi yake Arusha, Bw. Dennis Mburu katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Baada ya kupokea barua za utambulisho kutoka kwa Bw. Mburu Balozi Mulamula amemuahidi ushirikiano kutoka Serikalini wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini.
Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala ya biashara na uwekezaji pamoja na utalii.
WAZIRI MULAMULA APOKEA BARUA ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA KONSELI MKUU WA KENYA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 05, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 05, 2022
Rating:

Post a Comment