ZOEZI LA UBORESHAJI WA MITAALA NCHINI LINAENDELEA
Zoezi la uboreshaji wa Mitaala nchini likiwa linaendelea leo tarehe 13/09/2022 kamati ya mageuzi ya mfumo wa Elimu kutoka Zanzibar ikiongozwa na Mwenyekiti wake Prof Idris Ahmed Rai imekutana na kamati ya maboresho ya Mitaala inayongozwa na Prof.Makenya Maboko kwa lengo la kubadilisha uzoefu wa namna kazi ya uboreshaji Mitaala inavyofanyika.
Akiongoza kikao hicho kilichofanyika Jijini Dar es salaam Prof. Maboko amesema kuwa Serikali ina nia nzuri ya kufanya Mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu kwa upande wa bara na visiwani hivyo ni muhimu kamati hizi mbili kukaa kwa pamoja na kujadiliana mambo mbalimbali.
Kwa upande wake Prof.Idris amesema kuwa lengo la kufanya mazungumzo ni kuwa na lugha moja katika kutoa mapendekezo kuhusu maboresho ya mitaala.
Awali kabla ya kamati hizi mbili kukutana, kamati ya mageuzi ya mfumo wa Elimu kutoka Zanzibar walikutana na Menejimenti ya TET kwa lengo la kupata uelewa kuhusu majukumu ya TET na namna gani TET inavyoshirikiana na Zanzibar katika kuhakikisha ulinganifu wa Elimu unaotelewa.
ZOEZI LA UBORESHAJI WA MITAALA NCHINI LINAENDELEA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 13, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
September 13, 2022
Rating:




Post a Comment