Header AD

header ads

NAIBU KATIBU MKUU NDUGU JUMA MKOMI AFANYA KIKAO NA VIONGOZI WA USAID NA GIZ NCHINI.





Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma Mkomi amekutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Sekta za Maliasili na Mazingira wa Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID) Bw. Nathan pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Ujerumani nchini (GIZ), Dkt. Falconk. 

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa nyakati tofauti leo Septemba 13, 2022  jijini Dodoma, viongozi hao  wamejadili  namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya Maliasili na Utalii. Mkutano huo pia umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt. Maurus Msuha


NAIBU KATIBU MKUU NDUGU JUMA MKOMI AFANYA KIKAO NA VIONGOZI WA USAID NA GIZ NCHINI. NAIBU KATIBU MKUU NDUGU JUMA MKOMI AFANYA KIKAO NA VIONGOZI WA USAID NA GIZ NCHINI. Reviewed by Fahadi Msuya on September 13, 2022 Rating: 5