Balile: Waandishi wa habari tuandike na kuripoti habari zinazohusu tasnia ya habari
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Deodatus Balile amewataka Waandishi wa habari nchini kuandika na kuripoti habari na changamoto zinazohusu tasnia ya habari ili kusimama vyema na kutetea haki za waandishi wa habari nchini Tanzania.
Balile hayo Leo Alhamisi Oktoba 20, 2022 wakati wa semina ya kuwajengea uwezo Waandishi wa habari kuandika habari zinazohusu kampeni ya mchakato wa mabadiliko ya sheria ya habari ya mwaka 2016 ikiwa ni sehemu ya kufungua mradi wa kufanya uchechemuzi kwenye mabadiliko ya sheria hiyo.
Balile amesema waandishi wa habari wenyewe ndo wamavaa kiatu na wanahamu mazuri na mabaya wanayokutana nayo kwenye Tasnia hivyo wakiandika na kuyasemea matatizo wanayokutana nayo itaifanya dunia itambue changamoto za waandishi wa habari.
" Ili kutetea haki zetu zipatikane tukiwa na hali nzuri basi tutakua na nguvu ya kutetea haki za wengine kwa ufasaha pia tuondee ile kasumba ya kwamba wanahabari hatuandiki habari zinazotuhusu" amesema Balile
Balile amesema watawala wengi wanaogopa wananchi watapata uelewa wa mambo mbalimbali kupitia vyombo vya habari watakua na uwezo wa kuhoji mambo mbalimbali hivyo watawala wanaminya vyombo vya habari ili kufifisha maarifa kwa wananchi ili waendelee kutawala watu wasiokua na uelewa.
" Vyombo vya habari vina nafasi kubwa sana ya kubadilisha mitazamo na maisha ya watu kwa haki ya kupata habari ambayo hupelekea haki nyingine kupatikana " amesema Balile
Pia Balile amesema wakati mchakato wa marekebisho ya sheria ya huduma za habari ukiendelea ni vyema wanahabari wakazingatia weledi na nidhamu katika utendaji kazi ili kutumiza wajibu wa kuelimisha na kuhabarisha umma.
Kwa upande wake Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dkt. Wiebe De Boer ambaye alikua mgeni rasmi katika kikao hicho amepongeza Jukwaa la Wahariri TEF katika programu zao za kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kufanya kazi kwa weledi .
Amesema ubalozi wa Uholanzi uko tayari kusaidiaTEF katika mipango yake mbalimbali ya kuifanya tasnia ya habari kuwa bora zaidi.
Balile: Waandishi wa habari tuandike na kuripoti habari zinazohusu tasnia ya habari
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 20, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 20, 2022
Rating:




Post a Comment