Header AD

header ads

Mchakato wa mabadiliko ya sheria ya huduma za habari Balozi wa Uholanzi aipongeza TEF


Na Yusuph Digossi

Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dkt. Wiebe De Boer amelipongeza Jukwaa la Wahariri TEF katika programu zao za kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kufanya kazi kwa weledi .

Balozi De Boer ametoa pongezi hizo Leo Alhamisi Oktoba 20 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo Waandishi wa habari kuandika habari zinazohusu kampeni ya utetezi mabadiliko ya sheria ya habari ya mwaka 2016 iliyoratibiwa na TEF.



“Ninawapongeza TEF kwa juhudi za kutoa elimu juu ya maboresho ya habari kwani uhuru wa habari ni nguzo muhimu katika ustawi wa demokrasia pia demokrasia inategemea upatikanaji wa taarifa kwa uwazi na za kuaminika". amesema Balozi De Boer 

Amesema ubalozi wa Uholanzi uko tayari kusaidiaTEF katika mipango yake mbalimbali ya kuifanya tasnia ya habari kuwa bora zaidi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Deodatus Balile amewataka Waandishi wa habari nchini kuandika na kuripoti habari na changamoto zinazohusu tasnia ya habari ili kusimama vyema na kutetea haki za waandishi wa habari nchini Tanzania.




Mchakato wa mabadiliko ya sheria ya huduma za habari Balozi wa Uholanzi aipongeza TEF Mchakato wa mabadiliko ya sheria ya huduma za habari Balozi wa Uholanzi aipongeza TEF Reviewed by Fahadi Msuya on October 20, 2022 Rating: 5