BENKI YA EQUITY KUENDELEA KUVUTIA WAWEKEZAJI KUWEKEZA TANZANIA
Katika kuhakikisha wawekezaji kutoka nje wanakuja kuwekeza nchini, Benki ya Equity Tanzania imeratibu ziara ya kimkakati iliyofanywa na wawekezaji kutoka nchini Marekani wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania na Kenya .
Ziara hiyo inatazamiwa kufungua milango na nafasi kwa wafanyabiashara nchini Tanzania kupata nafasi ya kukuza soko la kuuza bidhaa nje ya mipaka ya Tanzania pamoja na kuungana na wananuzi kutoka maeneo mengine.
Wawekezaji hao wameonesha nia ya kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya, kilimo, usafirishaji na sekta nyingine ambazo zinatazamiwa kutengeneza fursa na kunufaisha pande zote mbili.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mwangalizi wa biashara kutoka Benki ya Equity, Adams Marandu amesema kuwa Benki hiyo inaendelea kuhakikisha wawekezaji kutoka nje wanakuja kuwekeza hapa nchini ili kutengeneza fursa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kukuza soko lao la kibiashara.
"Benki ya Equity imeendelea kuhakikisha wawekezaji kutoka nje wanakuja nchini kuwezekeza ili kuwawezesha wafanyabishara nchini kupata nafasi ya kukuza soko kwa kuuza bidhaa zao lakini pia kupata kuungana na wanunuzi katika maeneo mengine" amesema Marandu
Ameongeza kuwa "Tanzania ina eneo kubwa la Ardhi, nafasi kubwa ya vyanzo vya umwagiliaji kutokana na hilo, tunashirikisha wawekezaji kutoka Duniani lakini pia kutoka Afrika wanaotuzunguka kutoka Tanzania"
Kwa upande wake Mkurugenzi kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Zack Mbena amewataka wafanyabishara nchini kutumia vizuri fursa hiyo ya wawekezaji kutoka Marekani waliokuja nchini ili biashara zao kuwa na viwango lakini pia kuleta teknolojia hasa katika maeneo ya viwanda , TEHAMA na sekta ya huduma za kifedha.
Baadhi ya wawekezaji walioshiriki katika mkutano huo wamesema kuwa Tanzania imekua ni kitivo na mlango wa uwekezaji kutokana na sera na mazimgira yake yaliyopo,hivyo wanavutiwa kuwekeza katika nchi ambayo wana uhakika itazaa matunda katika uwekezaji wao.
BENKI YA EQUITY KUENDELEA KUVUTIA WAWEKEZAJI KUWEKEZA TANZANIA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 25, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 25, 2022
Rating:



Post a Comment