WWF YAWAPIGA MSASA TBA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIFEDHA ENDELEVU
Shirika la Uhifadhi wa Mazingira duniani , WWF Tanzania imewajengea uwezo taasisi za fedha ambazo wanachama wa umoja wa mabenki Tanzania (TBA) kwa lengo la kuhakikisha utoaji wa huduma za kifedha endelevu unaozingatia utunzaji wa mazingira, kuhusisha jamii pamoja na ukuaji wa uchumi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam wakati wa semina ya mafunzo ya wakuwajengea TBA Afisa Mradi wa " Regional Sustainable Investment Program" WWF Tanzania Happiness Minja amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kuchukua tahadhari za utunzaji wa mazingira, na kutatua changamoto za kijamii unaoenda sambamba katika mikopo ambayo Benki zimekua zikitoa kwa wawekezaji mbalimbali.
Amesema kupitia mafunzo hayo Benki zitakua na uwezo wa kumshauri Mwekezaji aliyeenda kuomba mkopo kuhusu athari za kimazingira zinazoweza kutokea wakati akitekeleza mradi wake kwasababu kuna baadhi ya miradi imekua ikiharibu mazingira.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Mabenki Tanzania TBA Tuse Mwaikasi amesema sasa ni wakati wa Tanzania kuungana na dunia katika utunzaji wa mazingira huku akibainisha kuwa katika kutekeleza dhana ya utoaji wa huduma za kifedha endelevu amezishauri benki zitoe mikopo ambayo itaenda kutekeleza miradi inayotunza mazingira na kutatua changamoto za jamii.
"Tunaona Sasa hivi kumekuwa na ukame, vyakula vinapungua, mafuriko, mifugo inapata shida kwahiyo kama sekta ya banki ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa tunakuwa na uelewa wa kutosha kwa kujua ni kiasi gani mikopo tunayotoa inaenda kuleta madhara kiasi gani katika mazingira yetu ili kwamba tusiwe sehemu ya kuchangia katika uharibifu wa mazingira yetu" amesema Tuse
WWF YAWAPIGA MSASA TBA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIFEDHA ENDELEVU
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 25, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 25, 2022
Rating:




Post a Comment